Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kujitahidi Kuwa Washindi
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 3. (a) Ni kitia-moyo gani ambacho Yesu aliwapa Wakristo katika Smirna? (b) Ingawa Wakristo katika Smirna walikuwa maskini, ni kwa nini Yesu alisema wao walikuwa ‘matajiri’?

      3 “Mimi najua dhiki na umaskini wako—lakini wewe u tajiri—na kufuru la wale ambao husema wao wenyewe ni Wayahudi, na kumbe wao sio bali ni sinagogi la Shetani.” (Ufunuo 2:9, NW)

  • Kujitahidi Kuwa Washindi
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 4. Wakristo katika Smirna walipatwa na upinzani mwingi sana kutoka kwa nani, naye Yesu aliwaonaje wapinzani hao?

      4 Yesu anataja hasa kwamba Wakristo katika Smirna wamechukuana na upinzani mwingi mikononi mwa Wayahudi wa kimnofu. Katika siku za mapema zaidi, wengi wa dini hii walipinga kwa dhati kuenea kwa Ukristo. (Matendo 13:44, 45, 14:19) Sasa, miongo michache tu baada ya Yerusalemu kuanguka, Wayahudi hao katika Smirna wanaonyesha roho ile ile ya kishetani. Si ajabu kwamba Yesu anawaona hao kuwa “sinagogi la Shetani”!a

  • Kujitahidi Kuwa Washindi
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Muda mfupi baada ya siku ya Bwana kuanza, maneno ya Yesu kwa Wakristo katika Smirna yalileta faraja halisi kwa kikundi kidogo cha kimataifa cha watu wa Yehova. (Ufunuo 1:10) Tangu 1879, hao walikuwa wamekuwa wakichimbua kutoka Neno la Mungu utajiri wa kiroho ambao wao walishiriki na wengine bila malipo. Lakini wakati wa Vita ya Ulimwengu 1, walikutana na chuki na upinzani mkali, kwa sehemu kwa sababu wao hawakujitia katika ile harara ya vita na kwa sehemu kwa sababu wao walikuwa wakifunua wazi bila woga makosa ya Jumuiya ya Wakristo. Ule mnyanyaso ambao wao walipokea ukichochewa na baadhi ya viongozi wa kidini wa Jumuiya ya Wakristo ulifikia upeo katika 1918 na ulilinganika na ule waliopokea Wakristo katika Smirna kutoka jamii ya Kiyahudi iliyokuwa huko.

      8 Wimbi moja la mnyanyaso katika United States ya Amerika lilifikia upeo wakati yule msimamizi mpya wa Sosaiti ya Mnara wa Mlinzi, Joseph F. Rutherford, na washiriki saba walipelekwa kwenye gereza katika Juni 22, 1918, walio wengi wao wakiwa na hukumu za kifungo cha miaka 20. Waliachiliwa kwa dhamana miezi tisa baadaye. Mei 14, 1919, mahakama ya rufani ilibadili hatia walizowekewa kimakosa; ilionyeshwa kulikuwako makosa 130 katika jaribio hilo. Jaji Manton, Mroma Katoliki, mwenye daraja la utawa wa Mtakatifu Gregori Mkuu, ambaye katika 1918 alikuwa amekataa dhamana kwa hao Wakristo, baadaye katika 1939, alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na faini ya dola 10,000 kwa mashtaka sita ya kuomba na kupokea rushwa.

      9. Mashahidi wa Yehova katika Ujeremani wa Nazi walitendwaje na Hitla, na kukiwa tendo-mwitikio gani kutoka viongozi wa kidini?

      9 Wakati wa utawala wa Nazi katika Ujeremani, Hitla alipiga marufuku kabisa kabisa kazi ya kuhubiri ya Mashahidi wa Yehova. Kwa miaka kadhaa, maelfu ya Mashahidi walifungwa ndani ya kambi za mateso na magereza kikatili, ambako wengi walikufa, huku wanaume vijana 200 ambao walikataa kupigana katika jeshi la Hitla wakifishwa kwa amri ya serikali. Uungaji-mkono wa viongozi wa kidini wa yote haya unathibitishwa na maneno ya padri Mkatoliki, yaliyochapishwa katika ile nyusipepa The German Way ya Mei 29, 1938. Kwa sehemu, yeye alisema: “Sasa kuna nchi moja duniani ambako wale wanaoitwa eti . . . Wanafunzi wa Biblia [Mashahidi wa Yehova] wamekatazwa. Hiyo ni Ujeremani! . . . Wakati Adolf Hitla alipochukua mamlaka, nayo Episkopati ya Kikatoliki katika Ujeremani ikarudia ombi lao, Hitla akasema: ‘Hawa wanaoitwa eti Wanafunzi wa Biblia [Mashahidi wa Yehova] Wenye Bidii ni wafanyiza matata; . . . mimi nawaona kuwa wadanganyaji; mimi sivumilii kwamba Wakatoliki Wajeremani watatupiwa matope jinsi hiyo na huyu Mwamerika Jaji Rutherford. Mimi nafumua [Mashahidi wa Yehova] katika Ujeremani.’” Kwa hayo, yule padri akaongeza: “Hongera!”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki