Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Falsafa ya Kigiriki—Je, Iliboresha Ukristo?
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Agosti 15
    • Plotinasi (205-270 W.K.), aliyetangulia watu hao wenye kufikiri, alitokeza mfumo ambao hasa ulitegemea nadharia ya mawazo ya Plato. Plotinasi alitokeza dhana ya nafsi iliyo tofauti na mwili. Profesa E. W. Hopkins alisema hivi kuhusu Plotinasi: “Theolojia yake . . . iliathiri sana viongozi wa maoni ya Kikristo.”

  • Falsafa ya Kigiriki—Je, Iliboresha Ukristo?
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Agosti 15
    • Wachafuzi Wenye Kufisidi

      Imeonekana kwamba “Waplato Wakristo walizingatia sana ufunuo na kuiona falsafa ya Plato kuwa kifaa bora zaidi cha kusaidia kuelewa na kutetea mafundisho ya Maandiko na mapokeo ya kanisa.”

      Plato mwenyewe alikuwa amesadiki kwamba kuna nafsi isiyoweza kufa. La muhimu ni kwamba kutokufa kwa nafsi ni mojawapo ya mafundisho maarufu yasiyo ya kweli yaliyojipenyeza katika “theolojia ya Ukristo.” Kukubali fundisho hili hakuwezi kuhalalishwa eti kwa sababu kufanya hivyo kuliufanya Ukristo uvutie zaidi umma. Alipokuwa akihubiri huko Athene, kitovu hasa cha utamaduni wa Kigiriki, mtume Paulo hakufundisha fundisho la Kiplato la nafsi. Badala yake, alihubiri fundisho la Kikristo la ufufuo, hata ingawa wasikilizaji wengi Wagiriki waliliona kuwa jambo gumu kukubali aliyosema.—Matendo 17:22-32.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki