-
Sherehe Ambazo Zinamchukiza Mungu“Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
-
-
ISTA—IBADA YA UWEZO WA KUZAA INAYOSINGIZIWA KUWA YA KIKRISTO
13, 14. Desturi za Ista zinazopendwa na wengi zilitoka wapi?
13 Ingawa inasemekana kwamba Ista ni maadhimisho ya ufufuo wa Kristo, ukweli ni kwamba inatokana na dini ya uwongo. Jina Ista limehusianishwa na Eostre, au Ostara, mungu wa mapambazuko na majira ya kuchipuka kwa majani aliyekuwa akiabudiwa na Wasaksoni wa kale wa Uingereza. Namna gani sungura na mayai yanayotumiwa wakati wa Ista? Kulingana na kitabu kimoja, mayai, “kwa muda mrefu yamekuwa yakiwakilisha uhai mpya na ufufuo,” naye sungura akiwakilisha uwezo wa kuzaa. Kwa hiyo, Ista ni maadhimisho ya kusherehekea uwezo wa kuzaa inayosingiziwa kuwa maadhimisho ya ufufuo wa Kristo.e
-
-
Sherehe Ambazo Zinamchukiza Mungu“Jitunzeni Katika Upendo wa Mungu”
-
-
e Pia, Ista alikuwa mungu wa kike wa uzazi. Kulingana na kamusi The Dictionary of Mythology, “Ista alikuwa na sungura mwezini ambaye alipenda mayai na nyakati nyingine alionyeshwa akiwa na kichwa cha sungura.”
-