-
Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye TamatiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
22 Babuloni Mkubwa “huketi juu ya maji mengi.” Kulingana na Ufunuo 17:1, 15, (NW), hayo hufananisha “vikundi vya watu na umati wa watu na mataifa na ndimi”—magenge ya wafuasi ambao yeye huwaona kuwa himaya. Lakini “maji” yanakauka! Katika Ulaya Magharibi, ambako hapo kwanza alikuwa na uvutano mwingi, mamia ya maelfu wamepuuza dini waziwazi. Katika mabara fulani, kwa miaka mingi kulikuwa na sera iliyojulishwa wazi kujaribu kuharibu uvutano wa dini. Matungamo katika mabara hayo hayakuinuka kumsaidia.
-
-
Kasirani ya Mungu Yaletwa Kwenye TamatiUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Katika Uingereza wakati wa miongo mitatu iliyopita, “karibu makanisa ya Kianglikana 2,000 kati ya yale 16,000 yamefungwa kwa sababu ya kutotumiwa. Hadhirina imepungua kuwa miongoni mwa zile za chini zaidi sana za nchi zinazokiri kuwa za Kikristo. . . . ‘Sasa hali ni kwamba Uingereza si nchi ya Kikristo,’ akasema [Askofu wa Durham].”—The New York Times, Mei 11, 1987, ukurasa A4.
“Baada ya saa nyingi za majadiliano makali, Bunge [la Ugiriki] liliidhinisha leo sheria itungwe, ikiiwezesha Serikali ya Kisoshalisti itwae mali zenye mashamba makubwa mno zinazoshikiliwa na Kanisa Orthodoksi la Ugiriki . . . Zaidi ya hilo, sheria hiyo inawapa wasio viongozi wa kanisa udhibiti wa mabaraza ya kanisa na halmashauri zenye madaraka ya kusimamia vitega-uchumi vya kanisa vyenye thamani kubwa kutia ndani mahoteli, mashimo ya kuchimba marumaru na majengo ya maofisi.”—The New York Times, Aprili 4, 1987, ukurasa 3.
-