-
Je, Jina Yehova Linapaswa Kuwa Katika Agano Jipya?Mnara wa Mlinzi—2008 | Agosti 1
-
-
Watafsiri Wameshughulikia Jambo Hilo Jinsi Gani?
Je, Tafsiri ya Ulimwengu Mpya ndiyo Biblia pekee inayotumia jina la Mungu inapotafsiri Maandiko ya Kigiriki? Hapana. Kutokana na uthibitisho uliotajwa, watafsiri wengi wa Biblia wameonelea kwamba jina la Mungu linapaswa kutumiwa katika kutafsiri Agano Jipya.
Kwa mfano, tafsiri nyingi za Agano Jipya katika lugha za Afrika, Asia, Marekani, na Visiwa vya Pasifiki, zimetumia jina la Mungu mara nyingi. (Ona chati kwenye ukurasa wa 21.) Baadhi ya tafsiri ni za karibuni kwa mfano, Biblia ya Rotuman (1999), inatumia jina Jihova mara 51 katika mistari 48 ya Agano Jipya, na tafsiri ya Batak-Toba (1989) kutoka Indonesia, inatumia jina Jahowa mara 110 katika Agano Jipya. Jina la Mungu linapatikana pia katika tafsiri za Kifaransa, Kihispania, na Kijerumani. Kwa mfano, Pablo Besson alitafsiri Agano Jipya katika Kihispania mapema katika karne ya 20. Tafsiri yake inatumia jina la Jehová kwenye Yuda 14, na maelezo ya chini 100 hivi yanapendekeza kwamba jina la Mungu lilipaswa kutumiwa.
Zifuatazo ni baadhi ya tafsiri za Kiingereza ambazo zimetumia jina la Mungu katika Agano Jipya:
A Literal Translation of the New Testament . . . From the Text of the Vatican Manuscript, ya Herman Heinfetter (1863)
The Emphatic Diaglott, ya Benjamin Wilson (1864)
The Epistles of Paul in Modern English, ya George Barker Stevens (1898)
St. Paul’s Epistle to the Romans, ya W. G. Rutherford (1900)
The Christian’s Bible—New Testament, ya George N. LeFevre (1928)
The New Testament Letters, ya J.W.C. Wand, Askofu wa London (1946)
-
-
Je, Jina Yehova Linapaswa Kuwa Katika Agano Jipya?Mnara wa Mlinzi—2008 | Agosti 1
-
-
[Sanduku katika ukurasa wa 21]
ORODHA YA LUGHA 99 ZINAZOTUMIA TETRAGRAMATONI KATIKA LUGHA ZA KIENYEJI KATIKA AGANO JIPYA
CHIHOWA: Kichoctaw
IÁHVE: Kireno
IEHOUA: Kimer
IEHOVA: Gilbertese; Kihawaii; Kihiri Motu; Kikerewo; Kimarquesa; Kimotu; Kipanaieti (Misima); Kirarotonga; Kitahiti; Kitoaripi; Kiwai
IEHOVAN: Kisaibai
IEOVA: Kikuanua; Kiwedau
IHOVA: Kianeityum
IHVH: Kifaransa
IOVA: Kimalekula (Kuliviu); Kimalekula (Pangkumu); Kimalekula (Uripiv)
JAHOWA: Kibatak-Toba
JAHUÈ: Kichacobo
JAKWE: (Ki)Sukuma
JAHVE: Kihungaria
JEHOBA: Kimentawai; Kipsigis
JEHOFA: Kitswana
JEHOVA: Kijerumani; Kikélé (Gabon); Kikroatia; Kinandi; Kinauruan; Kinukuoro; Kilele; (Kisiwa cha Manus)
JEHOVÁ: Kihispania
JEHÔVA: Kifang; Kitsimihety
JEHOVAH: Kiefik; Kiholanzi; Kiingereza; Kikalenjin; Kimalagasi; Kinarrinyeri; Kiojibwa
JEOVA: Kikusaie (Kikosraea)
JIHOVA: Kinaga (Angami); Kinaga (Konyak); Kinaga (Lotha); Kinaga (Mao); Kinaga (Ntenyi); Kinaga (Sangtam); Kirotuman
JIOUA: Kimortlock
JIOVA: Kifiji
JIWHEYẸWHE: Kigu (Alada)
SIHOVA: Kitonga
UYEHOVA: Kizulu
YAHOWA: Kithai
YAHVE: Kiila
YAVE: Kikongo
YAWE: Kibobangi; Kibolia; Kijaluo; Kimongo (Lolo); Lingala; (Lo)Ngandu; (Lo)Ntumba; (Ke)Sengele
YEHÓA: Kiawabakal
YEHOFA: Sotho Kusini
YEHOVA: (Ki)Kalanga; Kichokwe; Kichuana (Tlapi); Kilogo; Kiluba; Kilugbara; Kisanto (Bandari ya Hog); Kitiv; Kiumbundu; (Chi)Luimbi; (Chi)Lunda (Ndembu); (Chi)Luvale; (Isi)Xhosa
YEHOVAH: Kibube; Kimohawk; Kinguna (Efate); Kinguna (Tongoa)
YEHOWA: Kiga; Kilaotia; Kitshiluba; (Ki)Songe
YEKOVA: Kizande
YEOBA: Kikuba (Inkongo)
YEOHOWA: Kikorea
YHWH: Kiebrania
YOWO: Kilomwe
ZAHOVA: Kichin (Haka-Lai)
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 23]
MTAFSIRI ALIYEHESHIMU JINA LA MUNGU
Mnamo Novemba (Mwezi wa 11) 1857, Hiram Bingham wa Pili, mmishonari aliyekuwa na umri wa miaka 26, aliwasili pamoja na mke wake katika Visiwa vya Gilbert (vinavyojulikana sasa kama Kiribati). Meli ya wamishonari waliyotumia kusafiri ilifadhiliwa na michango midogo ya watoto Wamarekani waliohudhuria mafundisho ya kidini ya watoto yanayofanywa Jumapili (Siku ya Yenga). Meli hiyo iliitwa Morning Star na wafadhili wake ili kuonyesha kwamba wanaamini kuwa Kristo atatawala kwa miaka elfu.
“Bingham alikuwa na matatizo ya kiafya,” anasema Barrie Macdonald katika kitabu chake (Cinderellas of the Empire). “Alikuwa na matatizo ya tumbo mara nyingi, na tatizo la muda mrefu la koo ambalo liliathiri uwezo wake wa kuongea hadharani; uwezo wake wa kuona ulikuwa dhaifu hivi kwamba angeweza kusoma tu kwa muda wa saa mbili au tatu kwa siku.”
Hata hivyo, Bingham alikuwa ameazimia kujifunza lugha ya Gilbertese. Hilo halikuwa jambo rahisi. Alianza kwa kuuliza majina ya vitu mbalimbali. Baada ya kukusanya maneno kama elfu mbili hivi, alimlipa mmoja wa wageuzwa-imani dola moja kwa kila maneno mapya 100 ambayo angeongezea kwenye orodha hiyo.
Ustahimilivu wa Bingham ulikuwa na matokeo mazuri. Kufikia wakati alipolazimika kuondoka kwenye Visiwa vya Gilbert mnamo 1865 kwa sababu ya afya yake iliyokuwa ikizorota, alikuwa ameanzisha mbinu ya kuandika lugha hiyo na pia alikuwa ametafsiri vitabu vya Mathayo na Yohana. Aliporudi tena kwenye visiwa hivyo mwaka wa 1873, alikuja na tafsiri iliyokamilishwa ya Agano Jipya katika lugha ya Gilbertese. Alikaa tena kwa miaka mingine 17, na kufikia mwaka wa 1890 alikuwa ametafsiri Biblia nzima katika lugha hiyo.
Tafsiri ya Biblia ya Bingham bado inatumika huko Kiribati mpaka leo. Wale wanaoisoma wanatambua kwamba alitumia jina la Yehova (Iehova katika Gilbertese) mara elfu kadhaa katika Agano la Kale na pia mara zaidi ya 50 katika Agano Jipya. Kwa kweli, Hiram Bingham alikuwa mtafsiri aliyeheshimu jina la Mungu!
[Picha]
Hiram Bingham wa Pili
Biblia ya Bingham katika Lugha ya Gilbertese
[Hisani]
Top photos from Alfred M. Bingham’s book: “The Tiffany Fortune”
-