Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Biblia Iko Hai Hata Katika Lugha Iliyokufa
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Aprili 1
    • Tafsiri za Zamani Zaidi za Kilatini

      Lugha ya kwanza ya Roma ilikuwa Kilatini. Hata hivyo, mtume Paulo alipowaandikia Wakristo katika jiji hilo alitumia Kigiriki.a Hilo halikuwa tatizo kwa sababu watu wengi walizungumza lugha zote mbili. Wakaaji wengi wa Roma walitoka katika maeneo ya Asia ambako Kigiriki kilizungumzwa, kwa hiyo ilisemekana kwamba Roma lilikuwa kama jiji la Ugiriki. Watu walizungumza lugha tofauti-tofauti katika maeneo mbalimbali ya Milki ya Roma, lakini kadiri milki hiyo ilivyopanuka, ndivyo Kilatini kilivyozidi kuwa lugha muhimu. Kwa sababu hiyo, Maandiko Matakatifu yaliyokuwapo katika Kigiriki yalianza kutafsiriwa katika Kilatini. Inaelekea kazi hiyo ilianza huko Afrika Kaskazini katika karne ya pili W.K.

      Tafsiri hizo mbalimbali zinaitwa Vetus Latina, ama Tafsiri ya Kale ya Kilatini. Hakuna hati ya kale yenye Biblia nzima ya Kilatini ambayo imedumu mpaka leo. Yaelekea Vetus Latina hakikuwa kitabu kimoja kama inavyoonyeshwa na hati zinazopatikana na pia sehemu ambazo zimenukuliwa na waandishi wa kale. Badala yake, yaelekea kazi hiyo ya kutafsiri ilifanywa na watu kadhaa kutoka sehemu mbalimbali na wakati tofauti-tofauti. Kwa hiyo, Vetus Latina si kitabu kimoja bali ni mkusanyo wa tafsiri mbalimbali kutoka Kigiriki.

      Watu waliochukua hatua ya kutafsiri sehemu za Maandiko katika Kilatini bila kushirikiana na watafsiri wengine, walisababisha mvurugo kwa kadiri fulani. Mwishoni mwa miaka ya 300 W.K., mwanatheolojia Mkatoliki Agostino alisema kwamba “mtu yeyote aliyeweza kupata hati ya Kigiriki na aliyefikiri kwamba anajua lugha hizo mbili, hata kwa kiwango kidogo tu, alianza kuitafsiri” katika Kilatini. Agostino na wengine waliona kwamba kulikuwa na tafsiri nyingi sana na walitilia shaka usahihi wa tafsiri hizo.

  • Biblia Iko Hai Hata Katika Lugha Iliyokufa
    Mnara wa Mlinzi—2009 | Aprili 1
    • [Sanduku katika ukurasa wa 21]

      MANENO YANAYOENDELEA KUTUMIWA

      Katika Vetus Latina kulikuwa na maneno mengi yaliyotafsiriwa kutoka katika Kigiriki ambayo yanaendelea kutumiwa. Mojawapo ya maneno hayo ni di·a·theʹke, linalotafsiriwa “agano.” (2 Wakorintho 3:14) Kwa sababu hiyo, katika lugha nyingi Maandiko ya Kiebrania na ya Kigiriki yanaitwa Agano la Kale na Agano Jipya.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki