-
Uko Macho Kuelekea Nyakati Zetu?Mnara wa Mlinzi—1998 | Septemba 15
-
-
Kuponyoka Maafa Makubwa Yaliyotokezwa na Binadamu
Katika karne ya kwanza ya Wakati wetu wa Kawaida, Wakristo waliokuwa wakiishi Yerusalemu pia iliwabidi kuamua kama wangeyaacha makao yao. Kukimbia kutoka katika jiji hilo mwaka wa 66 W.K. kuliwaokoa na uharibifu ambao uliwapata wakazi wale wengine na maelfu ya Wayahudi ambao walikuwa wamekuja Yerusalemu kwa ajili ya Sikukuu ya Kupitwa ya mwaka wa 70 W.K. Watu zaidi ya milioni moja walikuwa ndani ya jiji hilo lenye kuta wakiadhimisha Sikukuu ya Kupitwa wakati jeshi la Roma lilipofanya isiwezekane kabisa kupata fursa ya kutoroka. Njaa kuu, kung’ang’ania mamlaka, na mashambulizi yenye ukatili ya Waroma yalitokeza vifo vya watu zaidi ya milioni moja.
Maafa makubwa yaliyokomesha maasi ya Wayahudi dhidi ya Waroma hayakuja bila kutangazwa. Miongo kadhaa mapema, Yesu Kristo alikuwa ametabiri kwamba Yerusalemu lingezingirwa. Yeye alisema hivi: “Wakati mwonapo Yerusalemu limezingirwa na majeshi yaliyopiga kambi, ndipo jueni kwamba kufanywa ukiwa kwalo kumekaribia. Ndipo waacheni wale walio katika Yudea waanze kukimbia hadi kwenye milima, na waacheni wale walio katikati yalo waondoke, na waacheni wale walio katika sehemu za mashambani wasiingie ndani yalo.” (Luka 21:20, 21) Maagizo hayo yalikuwa wazi, na wafuasi wa Yesu waliyachukua kwa uzito.
Mwanahistoria wa karne ya nne Eusebia Kaisaria aripoti kwamba Wakristo wa Yudea yote walitenda kulingana na onyo la Yesu. Waroma walipoacha kuzingira Yerusalemu kwa mara ya kwanza katika 66 W.K., Wakristo wengi Wayahudi walienda kuishi katika jiji la Wasio Wayahudi la Pella, katika mkoa wa Roma wa Perea. Kwa kuwa macho kuelekea nyakati zao na kutenda kulingana na onyo la Yesu, waliponyoka kule ambako kumeitwa “mojawapo ya kuzingira kwenye kuogofya zaidi katika historia yote.”
-
-
Ni Saa ya Kuamka!Mnara wa Mlinzi—1998 | Septemba 15
-
-
Ni Saa ya Kuamka!
“USIKOSEE kuhusu kizazi tunamoishi; kwetu sisi tayari ni saa ya kuamka kutoka usingizini.” (Waroma 13:11, Knox) Mtume Paulo aliandikia Wakristo katika Roma maneno hayo yapata miaka 14 kabla ya msiba mkuu wa mfumo wa mambo wa Kiyahudi katika 70 W.K. Kwa sababu walikuwa macho kiroho, Wakristo Wayahudi hawakuwa Yerusalemu wakati huo wenye hatari, hivyo waliponyoka kifo au utumwa. Lakini walijuaje kwamba walihitaji kuondoka katika jiji hilo bila kuingia humo tena?
Yesu Kristo alikuwa ameonya kwamba adui zao wangezingira Yerusalemu na kwamba wakazi wake wangeangamizwa kabisa. (Luka 19:43, 44) Baada ya hapo, Yesu aliwapa wafuasi wake waaminifu ishara yenye mambo mengi ambayo haikuwa ngumu kuitambua. (Luka 21:7-24) Kuhusu wale Wakristo walioishi Yerusalemu, kuacha jiji hilo kulimaanisha kuacha makao yao na kazi zao. Hata hivyo, uangalifu wao na kukimbia kwao kuliokoa uhai wao.
Yesu alipotabiri juu ya uharibifu wa Yerusalemu, wanafunzi wake walimuuliza hivi: “Ni wakati gani mambo haya yatakuwa, nayo itakuwa ni nini ishara ya kuwapo kwako na ya umalizio wa mfumo wa mambo?” (Mathayo 24:3) Katika kujibu kwake, Yesu alilinganisha kuwapo kwake kwa wakati ujao na kipindi kilichoongoza hadi kwenye Furiko la tufeni pote la siku za Noa. Yesu alionyesha kwamba Gharika ilimaliza watu waovu wote. (Mathayo 24:21, 37-39) Hivyo alionyesha kwamba Mungu angeingilia kati mambo ya binadamu tena. Kwa kadiri gani? Naam, kufikia hatua ya kuondoa ulimwengu au mfumo wote wa mambo ulio mwovu! (Linganisha 2 Petro 3:5, 6.) Je, hilo lingetokea wakati wetu?
-