-
“Wao Si Sehemu ya Ulimwengu”Mwabudu Mungu wa Pekee wa Kweli
-
-
Kitabu On the Road to Civilization—A World History chasema hivi kuhusu Wakristo wa awali: ‘Wakristo walikataa kufanya kazi fulani zilizofanywa na raia Waroma. Waliona kujiunga na jeshi kuwa kinyume cha imani yao. Hawakukubali vyeo vya kisiasa. Hawakumwabudu maliki.’
-
-
“Wao Si Sehemu ya Ulimwengu”Mwabudu Mungu wa Pekee wa Kweli
-
-
9. (a) Kwa nini Wakristo waliokuwa Yerusalemu walikimbia mnamo mwaka wa 66 W.K.? (b) Waliweka mfano gani bora?
9 Wanafunzi hawakujiingiza kamwe katika mapambano ya kisiasa na ya kijeshi. Wayahudi wa Yudea walimwasi Kaisari mnamo mwaka wa 66 W.K. Jeshi la Roma likazingira Yerusalemu mara moja. Wakristo waliokuwa katika mji huo walifanya nini? Walikumbuka shauri la Yesu kwamba watoke katika mji huo. Waroma walipoondoka kwa muda, Wakristo walivuka Mto Yordani na kukimbilia eneo la milimani huko Pela. (Luka 21:20-24) Wakristo waaminifu leo wanapaswa kuiga mfano wao wa kutounga mkono upande wowote.
-