-
Desturi za Krismasi-Je, Ni za Kikristo?Mnara wa Mlinzi—2000 | Desemba 15
-
-
Katika pindi hii, nacimiento (Mandhari ya kuzaliwa kwa Kristo) huwa yenye kutokeza sana. Ni nini kinachohusika katika pindi hii? Katika sehemu za umma na vilevile makanisani na nyumbani, mandhari hujengwa yakiwa na sanamu (kubwa au ndogo) zilizotengenezwa kwa kauri, mbao, au udongo. Sanamu hizo hufananisha Yosefu na Maria wakipiga magoti mbele za hori yenye kitoto kilichotoka tu kuzaliwa. Mara nyingi kunakuwa na wachungaji na Los Reyes Magos (“wanaume wenye hekima”). Mandhari hiyo huonyesha hori, na huenda kukawa na wanyama kadhaa ili kuikamilisha. Hata hivyo, sanamu iliyo muhimu zaidi ni mtoto mchanga aliyezaliwa, ambaye anaitwa kwa Kihispania el Niño Dios (Mtoto-Mungu). Sanamu ya mtoto huyo mchanga yaweza kuwekwa hapo kwenye Mkesha wa Krismasi.
-
-
Desturi za Krismasi-Je, Ni za Kikristo?Mnara wa Mlinzi—2000 | Desemba 15
-
-
Kichapo The Encyclopedia Americana chaeleza hivi: “Michezo ya kuigiza ya Kuzaliwa kwa Kristo ikawa sehemu ya sherehe ya Krismasi hapo awali . . . Inasemekana michezo hiyo ya kuigiza hori kanisani ilianzishwa na Mtakatifu Francis.” Michezo hii ya kuigiza inayokazia kuzaliwa kwa Kristo ilifanywa katika makanisa wakati Mexico ilipofanywa kuwa koloni. Ilipangwa na watawa wa kiume wa “Mtakatifu Francis” ili kufundisha Wahindi kuhusu Kuzaliwa kwa Kristo.
-