Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Wakati wa Kuja Kwa Mesiya Wafunuliwa
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • [Sanduku/Picha katika ukurasa wa 197]

      Artashasta Alianza Kutawala Lini?

      WANAHISTORIA hawakubaliani kuhusu mwaka ambao Mfalme Artashasta Mwajemi alianza kutawala. Wengine wamesema kwamba alianza kutawala mwaka wa 465 K.W.K. kwa kuwa baba yake, Shasta, alianza kutawala mwaka wa 486 K.W.K. na akafa katika mwaka wa 21 wa utawala wake. Lakini kuna uthibitisho wa kwamba Artashasta alikalia kiti cha ufalme mwaka wa 475 K.W.K. na kuanza mwaka wake wa kwanza wa utawala mwaka wa 474 K.W.K.

      Maandishi na sanamu za kuchongwa zilizofukuliwa huko Persepolisi, jiji kuu la Uajemi la kale zaonyesha kwamba Shasta alitawala pamoja na baba yake, Dario wa Kwanza. Ikiwa alitawala pamoja naye kwa miaka 10 kisha Shasta akatawala peke yake kwa miaka 11 baada ya Dario kufa mwaka wa 486 K.W.K., mwaka wa kwanza wa utawala wa Artashasta ungekuwa mwaka wa 474 K.W.K.

      Ushuhuda wa pili wahusisha Jenerali Themistoklesi wa Athene, ambaye aliyashinda majeshi ya Shasta mwaka wa 480 K.W.K. Baadaye alianza kuchukiwa na Wagiriki akashtakiwa uhaini. Themistoklesi alikimbia na kutafuta ulinzi kwenye makao ya kifalme ya Uajemi, ambapo alipokewa vema. Kulingana na mwanahistoria Mgiriki Thusidide, hilo lilitokea punde tu baada ya Artashasta “kuanza kutawala.” Mwanahistoria Mgiriki Diodorus Siculus akadiria kwamba Themistoklesi alikufa wapata mwaka wa 471 K.W.K. Kwa kuwa Themistoklesi alikuwa ameomba ajifunze Kiajemi kwa mwaka mmoja kabla ya kuongea na Mfalme Artashasta, lazima awe alifika Asia Ndogo kabla ya mwaka wa 473 K.W.K. Tarehe hiyo yaungwa mkono na kichapo Chronicle of Eusebius cha Jerome. Kwa kuwa Artashasta alianza “kutawala punde tu” baada ya Themistoklesi kufika Asia mwaka wa 473 K.W.K., msomi Mjerumani Ernst Hengstenberg alitaarifu katika kichapo chake kiitwacho Christology of the Old Testament kwamba Artashasta alianza kutawala mwaka wa 474 K.W.K., kama vichapo vingine visemavyo. Aliongeza kusema kwamba: “Mwaka wa ishirini wa Artashasta ni mwaka wa 455 kabla ya Kristo.”

      [Picha]

      Sanamu ya Themistoklesi

  • Wakati wa Kuja Kwa Mesiya Wafunuliwa
    Sikiliza Unabii wa Danieli!
    • Kwa kuwa Artashasta alianza “kutawala punde tu” baada ya Themistoklesi kufika Asia mwaka wa 473 K.W.K., msomi Mjerumani Ernst Hengstenberg alitaarifu katika kichapo chake kiitwacho Christology of the Old Testament kwamba Artashasta alianza kutawala mwaka wa 474 K.W.K., kama vichapo vingine visemavyo. Aliongeza kusema kwamba: “Mwaka wa ishirini wa Artashasta ni mwaka wa 455 kabla ya Kristo.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki