-
Jiji la Kale la Yerusalemu Liliharibiwa Mwaka Gani?—Sehemu ya KwanzaMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
Je, Maandishi ya Wanahistoria wa Kale Ni Sahihi?
Wanahistoria walioishi karibu na wakati ambapo jiji la Yerusalemu liliharibiwa wanatoa habari zinazotofautiana kuhusu wafalme wa Milki Mpya ya Babiloni.c (Ona sanduku “Wafalme wa Milki Mpya ya Babiloni.”) Mfuatano wao wa matukio haupatani na ule wa Biblia. Hata hivyo, maandishi yao yanategemeka kadiri gani?
Mbabiloni anayeitwa Berossus, ambaye alikuwa “kuhani wa Beli,” ni mmoja kati ya wanahistoria walioishi karibu na kipindi cha Milki Mpya ya Babiloni. Kitabu chake kinachoitwa Babyloniaca, ambacho aliandika yapata mwaka wa 281 K.W.K., kilipotea, na ni visehemu tu vya kitabu hicho ambavyo vimehifadhiwa katika maandishi ya wanahistoria wengine. Berossus alidai kwamba alitumia “vitabu ambavyo vilikuwa vimehifadhiwa kwa uangalifu sana huko Babiloni.”1 Je, maandishi yake yalikuwa sahihi? Fikiria mfano mmoja.
Berossus aliandika kwamba Mfalme Senakeribu wa Ashuru alitawala baada ya “ndugu [yake]”; na baada yake mwana wake [Esarhadoni akatawala kwa] miaka 8; kisha, Sammuges [Shamash-shuma-ukin] akatawala kwa miaka 21.” (Kitabu cha Tatu, 2.1, 4) Hata hivyo, hati za historia ya Babiloni zilizoandikwa muda mrefu kabla ya kipindi cha Berossus zinasema kwamba Senakeribu alitawala baada ya baba yake, Sargoni wa Pili, na si baada ya ndugu yake; Esarhadoni alitawala miaka 12, si miaka minane; naye Shamash-shuma-ukin akatawala miaka 20, si miaka 21. Ingawa msomi R. J. van der Spek, anakubali kwamba Berossus alichunguza maandishi ya mfuatano wa matukio ya Wababiloni, anaandika hivi: “Hilo halikumzuia kuongeza mambo yake na ufafanuzi wake.”2
Wasomi wengine wana maoni gani kumhusu Berossus? “Zamani Berossus alionwa kuwa mwanahistoria,” anasema S. M. Burstein, ambaye alifanya uchunguzi wa kina kuhusu maandishi ya Berossus. Hata hivyo, alimalizia kwa kusema hivi: “Kwa kuchunguza maandishi yake, tunaona kwamba yamepungukiwa kihistoria. Hata sasa, visehemu vya Babyloniaca vina makosa mengi kuhusu mambo rahisi ya hakika . . . Mwanahistoria hapaswi kufanya makosa kama hayo, lakini kusudi la Berossus’ halikuwa kuandika habari za kihistoria.”3
Kutokana na hayo, una maoni gani? Je, hesabu za Berossus zinapaswa kuonwa kuwa sahihi na zenye kutegemeka? Namna gani wanahistoria wengine wa kale, ambao mara nyingi, waliandika mfuatano wa matukio ya kihistoria wakitegemea maandishi ya Berossus? Je, kweli maelezo yao yanaweza kutegemeka?
Orodha ya Ptolemy
Orodha ya Majina ya Wafalme iliyoandikwa na mtaalamu wa nyota wa karne ya pili W.K. Claudius Ptolemy, inatumiwa pia kuunga mkono mwaka wa 587 K.W.K. Orodha ya wafalme ya Ptolemy inaonwa kuwa msingi wa mfuatano wa matukio ya historia ya kale, kutia ndani kipindi cha Milki Mpya ya Babiloni.
Ptolemy aliandika orodha yake miaka 600 hivi baada ya kipindi cha Milki Mpya ya Babiloni kuisha. Basi, aliamua jinsi gani mwaka ambao mfalme wa kwanza kwenye orodha yake alianza kutawala? Ptolemy alieleza kwamba kwa kutumia hesabu za wataalamu wa nyota, ambazo kwa kadiri fulani zilitegemea kupatwa kwa mwezi, “tumehesabu kurudi nyuma mpaka mwanzo wa utawala wa Nabonassar,” mfalme wa kwanza kwenye orodha yake.4 Hivyo, Christopher Walker wa Jumba la Makumbusho la Uingereza anasema kwamba orodha ya Ptolemy ilikuwa “mbinu iliyokusudiwa kuwapa wataalamu wa nyota mfuatano mzuri wa matukio,” bali “si kuwapa wanahistoria rekodi sahihi kuhusu kuinuka na kufa kwa wafalme.”5
“Kwa muda mrefu, wataalamu wa nyota wameona Orodha hiyo kuwa yenye kutegemeka,” anaandika Leo Depuydt, mmoja kati ya wasomi wanaomtetea sana Ptolemy, “lakini hilo halimaanishi kwamba lazima Orodha hiyo iwe inategemeka kihistoria.” Profesa Depuydt anaongeza hivi kuhusu orodha hiyo ya wafalme: “Kuhusiana na watawala wa kale [ambao wanatia ndani wafalme wa Milki Mpya ya Babiloni], Orodha hiyo inahitaji kulinganishwa na maandishi ya kikabari ili kujua wakati ambao kila mfalme alitawala.”6
‘Maandishi hayo ya kikabari’ ambayo yanatusaidia kuchunguza usahihi wa orodha ya kihistoria ya Ptolemy ni nini? Yanatia ndani mfuatano wa matukio ya Wababiloni, orodha ya wafalme, na mambo ya kiuchumi—ambayo yaliandikwa na waandishi walioishi wakati wa Milki Mpya ya Babiloni, au karibu na wakati huo.7
Orodha ya Ptolemy inalingana jinsi gani na maandishi ya kikabari? Sanduku lenye kichwa “Orodha ya Ptolemy Inatofautiana Jinsi Gani na Mabamba ya Kale?” (lililo hapa chini) linaonyesha sehemu ya orodha hiyo na kuilinganisha na hati nyingine za kale za maandishi ya kikabari. Ona kwamba Ptolemy anaorodhesha wafalme wanne tu katikati ya watawala wa Babiloni, Kandalanu na Nabonido. Hata hivyo Orodha ya Wafalme ya Uruk—ambayo ni sehemu ya maandishi ya kikabari—inaonyesha kwamba kulikuwa na wafalme saba katikati ya wafalme hao wawili wa Babiloni. Je, wafalme hao saba walitawala kwa vipindi vifupi visivyo na umaana wowote? Kulingana na maandishi ya kikabari kuhusu mambo ya kiuchumi, mmoja wao alitawala kwa miaka saba.8
Pia, kuna uthibitisho mkubwa kwenye hati za maandishi ya kikabari kwamba kabla ya utawala wa Nabopolasa (mfalme wa kwanza katika kipindi cha Milki Mpya ya Babiloni), mfalme mwingine (Ashur-etel-ilani) alitawala milki ya Babiloni kwa miaka minne. Pia, kwa zaidi ya mwaka mmoja, hakukuwa na mfalme katika nchi hiyo.9 Hata hivyo, habari hizo zote hazipo katika orodha ya Ptolemy.
Kwa nini Ptolemy hakuorodhesha watawala fulani? Inaelekea kwamba hakuwaona kuwa watawala halali wa Babiloni.10 Kwa mfano, hakuorodhesha Labashi-Marduk, ambaye alikuwa mfalme katika Milki Mpya ya Babiloni. Lakini kulingana na maandishi ya kikabari, kwa kweli wafalme ambao hawakuorodheshwa na Ptolemy walitawala milki ya Babiloni.
Kwa ujumla, orodha ya Ptolemy inaonwa kuwa sahihi. Lakini kwa kufikiria habari ambazo haikutaja, je, inapaswa kutumiwa kama msingi hakika wa mfuatano wa matukio ya kihistoria?
-
-
Jiji la Kale la Yerusalemu Liliharibiwa Mwaka Gani?—Sehemu ya KwanzaMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
c Milki Mpya ya Babiloni ilianza na utawala wa Nabopolasa, baba ya Nebukadneza, na ikaisha wakati wa utawala wa Nabonido. Kipindi hicho cha wakati kinawavutia wasomi kwa sababu kinatia ndani sehemu kubwa ya ile miaka 70 ya ukiwa.
-
-
Jiji la Kale la Yerusalemu Liliharibiwa Mwaka Gani?—Sehemu ya KwanzaMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
8. Sin-sharra-ishkun alitawala kwa miaka saba, na mabamba 57 ya udongo ya mfalme huyo yanayohusu mambo ya kiuchumi yalianza kuandikwa wakati alipoanza kutawala mpaka mwaka wa saba wa utawala wake. Ona kitabu Journal of Cuneiform Studies, Buku la 35, 1983, ukurasa wa 54-59.
9. Bamba la mambo ya kiuchumi C.B.M. 2152 liliandikwa mwaka wa nne wa utawala wa Ashur-etel-ilani. (Kitabu Legal and Commercial Transactions Dated in the Assyrian, Neo-Babylonian and Persian Periods—Chiefly From Nippur, cha A.T. Clay, 1908, ukurasa 74.) Pia, maandishi ya Harran Inscriptions of Nabonidus, (H1B), I, mstari wa 30, yanamworodhesha kabla ya Nabopolasa. (Anatolian Studies, Buku la Nane, mwaka wa 1958, ukurasa wa 35, 47.) Kwa habari kuhusu kipindi ambacho hakikuwa na mfalme, ona Chronicle 2, mstari wa 14, katika kitabu Assyrian and Babylonian Chronicles, ukurasa wa 87-88.
10. Wasomi fulani wanadai kwamba kuna wafalme ambao Ptolemy hakuwaorodhesha kwa sababu walikuwa na jina la cheo, “Mfalme wa Ashuru.” Wanasema aliorodhesha tu wafalme wa Babiloni. Hata hivyo, kama inavyoonyeshwa kwenye sanduku katika ukurasa wa 30, wafalme fulani walio katika orodha ya Ptolemy walikuwa pia na jina la cheo, “Mfalme wa Ashuru.” Mabamba yanayohusu mambo ya kiuchumi, barua za maandishi ya kikabari, na maandishi mengine yanaonyesha waziwazi kwamba wafalme Ashur-etel-ilani, Sin-shumu-lishir, na Sin-sharra-ishkun walitawala milki ya Babiloni.
-
-
Jiji la Kale la Yerusalemu Liliharibiwa Mwaka Gani?—Sehemu ya KwanzaMnara wa Mlinzi—2011 | Oktoba 1
-
-
[Chati/Picha katika ukurasa wa 29]
(Ona mpangilio kamili katika nakala iliyochapishwa)
WAFALME WA MILKI MPYA YA BABILONI
Ikiwa wanahistoria hawa wanategemeka, kwa nini hawapatani?
Wafalme
Nabopolasa
BEROSSUS m. 350-270 K.W.K.. (21)
POLYHISTOR 105-? K.W.K. (20)
JOSEPHUS 37-?100 W.K. (—)
PTOLEMY m. 100-170 W.K. (21)
Nebukadneza wa Pili
BEROSSUS m. 350-270 K.W.K. (43)
POLYHISTOR 105-? K.W.K. (43)
JOSEPHUS 37-?100 W.K. (43)
PTOLEMY m. 100-170 W.K. (43)
Amel-Marduk
BEROSSUS m. 350-270 K.W.K. (2)
POLYHISTOR 105-? K.W.K. (12)
JOSEPHUS 37-?100 W.K. (18)
PTOLEMY m. 100-170 W.K. (2)
Neriglissar
BEROSSUS m. 350-270 K.W.K. (4)
POLYHISTOR 105-? K.W.K. (4)
JOSEPHUS 37-?100 W.K. (40)
PTOLEMY m. 100-170 W.K. (4)
Labashi-Marduk
BEROSSUS m. 350-270 K.W.K. (miezi 9)
POLYHISTOR 105-? K.W.K. (—)
JOSEPHUS 37-?100 W.K. (miezi 9)
PTOLEMY m. 100-170 W.K. (—)
Nabonido
BEROSSUS m. 350-270 K.W.K. (17)
POLYHISTOR 105-? K.W.K. (17)
JOSEPHUS 37-?100 W.K. (17)
PTOLEMY m. 100-170 W.K. (17)
(#) = Kipindi (cha miaka) ambacho wafalme walitawala kulingana na wanahistoria wa kale
[Hisani]
Photograph taken by courtesy of the British Museum
-