-
MatangazoHuduma ya Ufalme—2002 | Desemba
-
-
Matangazo
◼ Toleo la vichapo la Desemba: Yule Mtu Mkuu Zaidi Aliyepata Kuishi. Ikiwa hakuna toleo hilo, vitabu vifuatavyo vinaweza kutumiwa, Biblia—Neno la Mungu au la Binadamu?, Kitabu Changu cha Hadithi za Biblia, au Unaweza Kuishi Milele Katika Paradiso Duniani. Januari: Kitabu chochote kilichochapishwa kabla ya 1988 chenye kurasa 192 chaweza kutolewa. Makutaniko ambayo hayana vitabu vya zamani vyenye kurasa 192 yanaweza kutoa kitabu Jitihada ya Ainabinadamu ya Kutafuta Mungu au Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu! Februari: Kitabu kipya Mkaribie Yehova. Machi: Ujuzi Uongozao Kwenye Uhai Udumuo Milele. Jitihada ya pekee yapaswa kufanywa ili kuanzisha mafunzo ya Biblia ya nyumbani.
◼ Mialiko ya Ukumbusho ya 2003 katika lugha kuu ya kila kutaniko itatumwa hivi karibuni. Ikiwa kuna lugha nyingine katika eneo lenu na mngependa mialiko ya lugha hizo, yapasa kuombwa mara moja katika Fomu ya Kuomba Vitabu (S-14). Mialiko ya Ukumbusho yapatikana katika Kiarabu, Kichina (Sahili), Kifaransa, Kiganda, Kigujarati, Kihindi, Kiingereza, Kipunjabi, Kirundi, na Kiswahili. Tafadhali ombeni tu lugha zile zinazohitajiwa katika eneo lenu.
◼ Tafadhali tunawajulisha kwamba Ukumbusho wa mwaka wa 2004 utakuwa Jumapili, Aprili 4, baada ya jua kutua. Taarifa hii imetolewa mapema ili akina ndugu waweze kukodi au kufanya maagano yanayohitajiwa ili kupata majumba mahali ambako makutaniko kadhaa yanatumia Jumba moja la Ufalme na hivyo inawalazimu kutafuta majengo mengine. Wazee wanapaswa kufanya mapatano pamoja na wasimamizi wa jengo kuhakikisha kwamba hakutakuwa na usumbufu kutokana na utendaji mwingine katika jengo hilo ili mwadhimisho wa Ukumbusho uweze kuendelea kwa njia ya amani na kwa utaratibu. Kwa sababu ya umuhimu wa tukio hili, baraza la wazee linapochagua msemaji wa Ukumbusho, lapaswa kumteua mmojawapo wa wazee wenye kustahili zaidi badala ya kupokezana zamu tu au kutumia ndugu yuleyule kila mwaka, isipokuwa tu kuwe na mzee mwenye uwezo aliye mmoja wa watiwa-mafuta ambaye anaweza kutoa hotuba hiyo.
◼ Wahubiri wote waliobatizwa wanaohudhuria Mkutano wa Utumishi wa juma la Januari 6 wanaweza kupewa Kadi ya Mwelekezo wa Mapema Kuhusu Tiba/Ondoleo la Hatia na Kadi ya Utambulisho kwa ajili ya watoto wao.
◼ Njia ya kuongoza Shule ya Huduma ya Kitheokrasi wakati wa ziara ya mwangalizi wa mzunguko inafanyiwa marekebisho. Kuanzia Januari 2003, baada ya wimbo na sala ya kufungua, shule itafanywa kwa dakika 25 hivi. Kutakuwako na hotuba ya dakika tano kuhusu sifa ya usemi, hotuba ya Maagizo ya dakika kumi, na mambo makuu ya usomaji wa Biblia ya dakika kumi. Hotuba Namba 2, 3, na 4 hazitatolewa. Kisha utafuata Mkutano wa Utumishi kwa nusu saa. Baada ya wimbo, kutakuwako programu ya mwangalizi wa mzunguko, kisha wimbo na sala ya kumalizia.
◼ Ingawa zamani mwangalizi wa Shule ya Huduma ya Kitheokrasi alikuwa akiweka Karatasi za Shauri la Usemi kwenye faili yake, jambo hilo halitafaa tena, kwa kuwa fomu za shauri la usemi ziko kwenye vitabu. Kwa hiyo, kila mwangalizi wa shule atahitaji kutengeneza rekodi yake mwenyewe ya kuchunguza maendeleo ya wanafunzi. Ofisi ya tawi haitatoa rekodi yoyote ya pekee kwa kusudi hilo.
◼ Hotuba Namba 3 na Namba 4 katika Shule ya Huduma ya Kitheokrasi zitatoka kwenye kitabu Kutoa Sababu. Vichwa vidogo na ufafanuzi havihesabiwi pamoja na mafungu.
◼ Kuhesabiwa kwa vichapo na magazeti yote yaliyopo kwapaswa kufanywa Desemba 31, 2002 au karibu iwezekanavyo na tarehe hiyo. Hesabu hiyo ni kama ile inayofanywa kila mwezi na mratibu wa vitabu, na jumla zapasa kuandikwa kwenye fomu ya Orodha ya Vitabu (S-18-SW). Jumla ya idadi ya magazeti yaliyopo inaweza kupatikana kutoka kwa watumishi wa magazeti katika kila kutaniko kwenye kikundi cha vitabu. Kila kutaniko linaloratibu litapokea nakala tatu za fomu ya Orodha ya Vitabu (S-18-SW). Tafadhali tumeni nakala ya awali kwa ofisi kabla ya Januari 6. Wekeni nakala ya kaboni kwenye faili zenu. Nakala ya tatu inaweza kutumiwa ili kufanyia hesabu. Mwandishi wa kutaniko linaloratibu apaswa kusimamia kazi hiyo ya kuhesabu vichapo. Mwandishi na mwangalizi-msimamizi wa kutaniko linaloratibu watatia sahihi fomu hiyo.
-
-
Kwa Kweli Ingefaa Uitazame Video No Blood—Medicine Meets the ChallengeHuduma ya Ufalme—2002 | Desemba
-
-
Kwa Kweli Ingefaa Uitazame Video No Blood—Medicine Meets the Challenge
Una habari kadiri gani kuhusu njia nyingine mbalimbali za matibabu yasiyohusisha damu? Je, unaelewa baadhi ya vitu vinavyoweza kutumiwa badala ya damu na jinsi vinavyofanya kazi? Tazama video hii na utahini ujuzi wako kwa maswali yafuatayo.—Kwa sababu video hii ina sehemu fupi zinazoonyesha upasuaji, wazazi wanapaswa kutumia busara wanapoitazama pamoja na watoto wao wadogo.
(1) Ni sababu gani kuu inayofanya Mashahidi wa Yehova wakatae kutiwa damu mishipani, nayo yapatikana wapi katika Biblia? (2) Kuhusu matibabu, tungependa nini? (3) Wagonjwa wana haki gani ya msingi? (4) Kwa nini ni jambo la kiakili na la kudhamiria kukataa kutiwa damu mishipani? (5) Mtu anapopoteza damu nyingi sana, ni mambo gani mawili ambayo madaktari wanapaswa kufanya haraka? (6) Ni hatari zipi za kitiba zinazohusiana na kutiwa damu mishipani? (7) Taja baadhi ya vifaa ambavyo wapasuaji wanaweza kutumia ili kupunguza umwagikaji wa damu nyingi wakati wa upasuaji? (8) Ungependa kujulishwa nini kuhusu tiba yoyote inayoweza kutumiwa badala ya damu? (9) Je, upasuaji tata waweza kufanywa bila kutumia damu? (10) Madaktari wengi wako tayari kuwafanyia Mashahidi wa Yehova nini, na huenda wagonjwa wote wakatibiwa vipi wakati ujao?
Bila shaka itasaidia kuitazama video No Blood pamoja na wanafunzi wa Biblia, wenzi wa ndoa au watu wa ukoo wasio Mashahidi, wafanyakazi wenzako, walimu, na wanashule wenzako ambao huenda wakauliza maswali kuhusu msimamo wetu kuhusiana na damu. Kukubali matibabu yoyote yaliyoonyeshwa katika video hii ni uamuzi wa mtu binafsi na dhamiri yake.—Ona “Maswali Kutoka kwa Wasomaji” katika toleo la Mnara wa Mlinzi la Juni 15 na Oktoba 15, 2000.
-
-
Ripoti Ya Utumishi Ya AgostiHuduma ya Ufalme—2002 | Desemba
-
-
Ripoti Ya Utumishi Ya Agosti
Wast. Wast. Wast. Wast.
Idadi ya: Saa Mag. Z. K. Maf. Bi.
B
Pai. Pekee 69 134.1 8.9 77.2 14.4
Mapai. 443 66.5 2.8 31.3 6.0
Pai. Msai. 255 54.1 1.6 21.5 4.0
Wahu. 3,839 17.2 0.8 7.3 1.7
JUMLA 4,606 Kilele Kipya: 4,542
ER
Pai. Msai. 15 59.8 1.3 12.7 0.6
Wahu. — 14.5 0.4 4.6 0.4
K
Pai. Pekee 334 121.5 33.7 52.0 10.2
Mapai. 1,983 61.2 16.1 19.8 4.1
Pai. Msai. 597 52.4 12.5 15.2 2.8
Wahu. 14,475 13.7 4.9 4.4 1.0
JUMLA 17,389 Kilele Kipya: 17,138
S
Pai. Msai. 49 44.8 5.9 26.0 3.0
Wahu. — 11.1 2.5 8.7 1.6
T
Pai. Pekee 155 122.3 51.0 58.0 9.1
Mapai. 1,353 56.1 15.6 22.2 3.7
Pai. Msai. 347 51.9 14.1 17.9 3.3
Wahu. 9,228 12.8 5.3 5.4 1.0
JUMLA 11,083 Kilele Kipya: 11,083
U
Pai. Pekee 87 130.4 47.7 81.3 13.2
Mapai. 252 60.1 17.9 29.1 5.0
Pai. Msai. 135 54.3 15.8 25.3 4.5
Wahu. 2,790 11.5 5.0 5.6 1.2
JUMLA 3,264 Kilele Kipya: 3,080
-