Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Sauli—Chombo-Kichaguliwa kwa Bwana
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Mei 15
    • Kuzaliwa kwa Sauli akiwa Mroma kulimaanisha kwamba mmoja kati ya wazazi wake wa kiume wa kale alikuwa amepata pendeleo la kuwa raia wa Roma. Jinsi gani? Kuna njia kadhaa. Mbali na kuurithi, uraia ungeweza kupewa watu mmoja-mmoja au vikundi vya watu ama kwa sababu ya wema fulani mahususi, ama kwa sababu ya faida tu za kisiasa, au utumishi fulani wa pekee uliotolewa kwa Serikali. Mtumwa aliyeweza kulipa fedha ili awekwe huru na Mroma, au yule ambaye angewekwa huru na raia Mroma, angekuwa Mroma pia. Vivyo hivyo na askari-mstaafu wa jeshi la Roma. Baada ya muda, wenyeji waliokuwa wakiishi katika koloni za Roma wangeweza kuwa raia. Hata imesemwa kwamba katika nyakati fulani uraia ulinunuliwa kwa pesa nyingi sana. Jinsi ambavyo familia ya Sauli ilipata uraia ni jambo lisilofahamika.

  • Sauli—Chombo-Kichaguliwa kwa Bwana
    Mnara wa Mlinzi—1999 | Mei 15
    • Usajili na Utoaji wa Vyeti kwa Raia Waroma

      Usajili wa watoto halali wa raia wa Roma ulianzishwa na Augusto kwa sheria mbili zilizotungwa mwaka wa 4 na wa 9 W.K. Watoto walihitaji kusajiliwa kabla ya siku 30 baada ya kuzaliwa. Familia zilipaswa kufanya tangazo mbele ya hakimu kwenye ofisi ifaayo ya kuweka rekodi za umma katika mikoa, zikitaarifu kwamba mtoto huyo hakuwa haramu na kwamba alikuwa ni raia wa Roma. Majina ya wazazi, jinsia yake na jina lake, na tarehe aliyozaliwa pia ziliandikwa. Hata kabla ya kuanzishwa kwa sheria hizi, usajili wa raia wote katika manispaa, koloni, na wilaya zote za Roma ulifanywa upya kwa kuhesabu watu baada ya kila miaka mitano.

      Hadhi ya mtu ingeweza kuthibitishwa kwa kuchunguza maandishi yake katika hifadhi za nyaraka zilizotunzwa vyema. Nakala halali za maandishi hayo zingeweza kupatikana kwenye mabamba madogo ya mbao yenye kukunjwa. Wasomi wengi wanasema kwamba Paulo alipodai kuwa raia Mroma, huenda aliweza kuonyesha cheti cha kuthibitisha jambo hilo. (Matendo 16:37; 22:25-29; 25:11) Kwa kuwa uraia wa Roma ulionwa kuwa “mtakatifu” na ulimwezesha mtu kuwa na mapendeleo mengi, ughushi wowote wa vyeti hivyo ulikuwa kosa zito. Adhabu kwa sababu ya udanganyifu wowote juu ya hadhi ya mtu ilikuwa kifo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki