-
Usafi—Kwa Nini Ni Muhimu?Mnara wa Mlinzi—2008 | Desemba 1
-
-
Mama yake akiwa jikoni, anamsikia Max akiingia na anamletea sahani ya wali moto na maharagwe. Lakini anakunja uso anapoona mfuko juu ya meza safi. Anamwangalia mwana wake na kusema, “Maaaax!” Mwana wake anaelewa, anaondoa mfuko huo, na anakimbia kunawa mikono yake. Muda si muda, anarudi kula mlo ambao amekuwa akingoja kwa hamu. “Pole Mama. Nilisahau,” anasema.
Mama anayejali anaweza kufanya mengi katika kudumisha afya na usafi, ingawa anahitaji ushirikiano kutoka kwa familia yote. Kama kisa cha Max kinavyoonyesha, mazoezi ya muda mrefu yanahitajika kwa sababu usafi unahitaji jitihada nyingi na watoto wanahitaji kukumbushwa mara nyingi.
Mama ya Max anatambua kwamba chakula kinaweza kupata uchafu kwa njia nyingi. Hivyo, ananawa mikono kwa uangalifu kabla ya kushika chakula na pia anafunika chakula ili kuzuia kisichafuliwe na wadudu. Kwa kuhakikisha kwamba chakula kinahifadhiwa vizuri na nyumba ni safi na nadhifu, hasumbuliwi sana na panya au mende.
Sababu moja inayomfanya mama ya Max awe mwangalifu sana ni kwamba anataka kumpendeza Mungu. “Biblia inasema kwamba ni lazima watu wa Mungu wawe watakatifu kwa sababu Mungu ni mtakatifu,” anaeleza mama ya Max. (1 Petro 1:16) “Utakatifu ni sawa na usafi,” anaongeza. “Hivyo ninataka nyumba yangu iwe safi, na ninataka familia yangu iwe safi. Bila shaka, hilo linawezekana tu kwa sababu kila mtu katika familia anasaidia.”
-
-
Usafi—Kwa Nini Ni Muhimu?Mnara wa Mlinzi—2008 | Desemba 1
-
-
[Picha katika ukurasa wa 10]
Mama anayejali anaweza kufanya mengi katika kudumisha usafi wa familia yake
-