-
“Vitu vya Kuchukiwa na Mataifa Yote”Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Kutumia Harara ya Wakati wa Vita ili Kutimiza Malengo Yao
Huku kukiwa na harara ya utukuzo wa taifa uliokumba ulimwengu wakati wa vita ya ulimwengu ya kwanza, silaha mpya ilipatikana ili itumiwe dhidi ya Wanafunzi wa Biblia. Uadui wa viongozi wa kidini wa Protestanti na Katoliki ya Roma ungeweza kuonyeshwa kwa kutumia kisitiri cha uzalendo. Walitumia msisimko wa wakati wa vita kwa faida yao ili kuwashtaki Wanafunzi wa Biblia kuwa wachochezi—shtaka lilelile ambalo lilielekezwa kwa Yesu Kristo na mtume Paulo na viongozi wa kidini wa Yerusalemu wa karne ya kwanza. (Luka 23:2, 4; Mdo. 24:1, 5) Bila shaka, ili makasisi wafanye shtaka hilo, wao wenyewe wangelazimika kuwa waungaji mkono walio watendaji wa vita, lakini hilo halikuonekana kuwa likiwasumbua wengi wao, hata ingawa lilimaanisha kutuma vijana wakawaue washiriki wa dini yao wenyewe katika nchi nyingine.
Ilikuwa katika Julai 1917, baada ya kifo cha Russell, kwamba Watch Tower Society ilitoa kitabu The Finished Mystery, ufafanuzi juu ya Ufunuo na Ezekieli pamoja na Wimbo Ulio Bora. Kitabu hicho kilifunua waziwazi unafiki wa makasisi wa Jumuiya ya Wakristo! Kiligawanywa sana kwa wakati mfupi. Mwishoni mwa Desemba 1917 na mapema katika 1918, Wanafunzi wa Biblia katika Marekani na Kanada pia walianza kugawanya nakala 10,000,000 za ujumbe wenye kuchoma katika trakti The Bible Students Monthly. Trakti hiyo ya kurasa nne yenye ukubwa wa kiasi ilikuwa na kichwa “Kuanguka kwa Babiloni,” na ilikuwa na kichwa kidogo “Sababu Kwa Nini Ni Lazima Jumuiya ya Wakristo Iteseke Sasa—Tokeo la Mwisho.” Ilitambulisha matengenezo ya kidini ya Katoliki na Protestanti yakiwa pamoja kuwa Babiloni ya kisasa, ambayo lazima ianguke hivi karibuni. Katika kuunga mkono yale yaliyosemwa, ilitokeza tena kutoka kitabu The Finished Mystery mafafanuzi juu ya unabii mbalimbali unaoonyesha hukumu ya kimungu dhidi ya “Babiloni wa Kifumbo.” Kwenye ukurasa wa nyuma kulikuwa na katuni iliyochorwa kuonyesha ukuta ukiporomoka. Mawe makubwa kutoka kwenye ukuta huo yalikuwa na vibandiko kama vile “Fundisho la Utatu (‘3 X 1 = 1’),” “Kutokufa kwa Nafsi,” “Nadharia ya Mateso ya Milele,” “Uprotestanti—mafundisho, makasisi, n.k.,” “Uroma—mapapa, makadinali, n.k., n.k.”—na mawe hayo yote yalikuwa yakianguka.
Makasisi walighadhibishwa na kufunuliwa huko, kama vile makasisi wa Kiyahudi walivyoghadhibika wakati Yesu alipofunua unafiki wao. (Mt. 23:1-39; 26:3, 4) Katika Kanada makasisi walitenda upesi. Katika Januari 1918, makasisi zaidi ya 600 wa Kanada walitia sahihi ombi lenye kusihi serikali izuie vichapo vya Shirika la Kimataifa la Wanafunzi wa Biblia. Kama ilivyoripotiwa katika Winnipeg Evening Tribune, baada ya Charles G. Paterson, pasta wa Kanisa la St. Stephen katika Winnipeg, kushutumu kutoka kwenye mimbari The Bible Students Monthly, iliyokuwa na makala “Kuanguka kwa Babiloni,” Mkuu wa Sheria Johnson aliwasiliana naye ili apate nakala. Punde baadaye, Februari 12, 1918, amri ya serikali ya Kanada ilifanya liwe kosa linalostahili adhabu ya kutozwa faini na kufungwa gerezani, mtu akipatikana ana ama kitabu The Finished Mystery ama trakti inayoonyeshwa juu.
-
-
“Vitu vya Kuchukiwa na Mataifa Yote”Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Ripoti ndefu ya mhadhara huo ilichapwa siku iliyofuata katika gazeti Morning Tribune la Los Angeles. Makasisi walighadhibishwa sana hivi kwamba shirika la wahudumu lilifanya mkutano siku iyo hiyo na likamtuma msimamizi walo kwa mameneja wa gazeti hilo ili kuwajulisha juu ya kuudhika kwao kwingi. Kufuatia hilo, kulikuwa na kipindi cha kupekuliwapekuliwa kwa ofisi za Watch Tower Society na washiriki wa idara ya upelelezi ya serikali.
Wakati wa kipindi hicho cha harara ya utukuzo wa taifa, kongamano la makasisi lilifanywa jijini Philadelphia, katika Marekani, ambamo azimio lilipitishwa likiomba Sheria ya Ujasusi ipitiwe tena ili wakiukaji wanaoshtakiwa wajaribiwe katika mahakama ya kijeshi na kupewa adhabu ya kifo. John Lord O’Brian katibu wa pekee wa mkuu wa sheria kwa kazi ya vita, aliteuliwa kuwasilisha jambo hilo katika Bunge. Rais wa Marekani hakuruhusu mswada huo uwe sheria. Lakini Meja-Jenerali James Franklin Bell, wa jeshi la Marekani, akiwa ameghadhibika sana aliwaambia J. F. Rutherford na W. E. Van Amburgh yale yaliyokuwa yametukia kwenye kongamano hilo na kusudi la kutumia mswada huo dhidi ya maofisa wa Watch Tower Society.
-
-
“Vitu vya Kuchukiwa na Mataifa Yote”Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Katika Worcester, Massachusetts, “Mwadhama” B. F. Wyland alitumia harara ya vita kwa faida yake kwa kudai kwamba Wanafunzi wa Biblia walikuwa wakiendeleza propaganda ya adui. Alichapa makala moja katika Daily Telegram ambayo alijulisha: “Mojawapo kazi za uzalendo zinazowakabili nyinyi mkiwa wananchi ni kulikandamiza Shirika la Kimataifa la Wanafunzi wa Biblia, lenye makao makuu katika Brooklyn. Chini ya kisitiri cha dini, wamekuwa wakiendeleza propaganda ya Ujerumani katika Worcester kwa kuuza kitabu chao, ‘The Finished Mystery.’” Aliwaambia wenye mamlaka waziwazi kwamba ilikuwa kazi yao kuwakamata Wanafunzi wa Biblia na kuwazuia wasifanye mikutano zaidi.
Kulikuwa na mnyanyaso wenye kuenea wa Wanafunzi wa Biblia katika masika na kiangazi cha 1918, katika Amerika Kaskazini na Ulaya pia. Miongoni mwa wachochezi mlikuwamo makasisi wa Baptisti, Methodisti, Episkopali, Luther, Katoliki ya Roma, na makanisa mengineyo.
-
-
“Vitu vya Kuchukiwa na Mataifa Yote”Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Kesi ilianza Juni 5, washtaki wakiwa Isaac R. Oeland na Charles J. Buchner wa Katoliki ya Roma. Wakati kesi ilipokuwa ikiendelea, kama vile Ndugu Rutherford alivyoona, mapadri Wakatoliki walishauriana mara kwa mara na Buchner na Oeland.
-
-
“Vitu vya Kuchukiwa na Mataifa Yote”Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Hata hivyo, inastahili kuangaliwa pia kwamba kabla ya kupitisha hukumu, Hakimu Howe alisema kwamba taarifa zilizotolewa na mawakili wa washtakiwa zilikuwa zimetia shuku na kutendea isivyofaa si maofisa wa sheria wa serikali tu bali pia “wahudumu wote wa kidini kotekote nchini.”
-