Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • 21. (a) Wale maadui wa kidini wa mashahidi wawili walitumiaje kwa faida yao hali ya vita? (b) Uhakika wa kwamba zile maiti za mashahidi wawili ziliachwa bila kuzikwa ulionyesha nini? (c) Kipindi cha wakati cha siku tatu na nusu chapasa kionweje? (Ona kielezi cha chini.)

      21 Kutoka 1914 kufika 1918 mataifa yalikuwa yakishughulika na vita ya kwanza ya ulimwengu. Hisi za utukuzaji wa taifa zilipanda juu, na katika masika ya 1918, maadui wa kidini wa mashahidi wawili walijifaidi na hali hiyo. Walitumia kwa hila chombo cha Serikali cha kisheria hivi kwamba wahudumu wenye madaraka miongoni mwa Wanafunzi wa Biblia walitiwa gerezani kwa mashtaka bandia ya kufitini serikali. Wafanya kazi wenzi waaminifu waliduwaa.

  • Kuhuisha Mashahidi Wawili
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Katika kitabu chake Preachers Present Arms, kilichotangazwa katika 1933, Ray H. Abrams anarejezea upinzani mkali wa viongozi wa kidini kuelekea kitabu cha Wanafunzi wa Biblia The Finished Mystery. Yeye hupitia jitihada za viongozi wa kidini za kuondolea mbali Wanafunzi wa Biblia na “usadikishi [wao] wenye kusumbua sana.” Hiyo iliongoza kwenye kesi ya mahakamani iliyokuwa na tokeo la kuhukumia J. F. Rutherford na waandamani wenzake saba miaka mirefu gerezani. Dakt. Abrams anaongezea: “Uchanganuzi wa kesi yote hiyo unaongoza kwenye mkataa wa kwamba makanisa na viongozi wa kidini mwanzoni ndio walioanza mwendo wa kufutilia mbali Waruseli. Katika Kanada, katika Februari, 1918, makasisi walianza kampeni kamili dhidi yao na vichapo vyao, hasa The Finished Mystery. Kulingana na Tribune ya Winnipeg, . . . kukandamizwa kwa kitabu chao kuliitikadiwa kuwa kuliletwa moja kwa moja na ‘mawakilisho ya viongozi wa kidini.’”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki