Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Vitu vya Kuchukiwa na Mataifa Yote”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Hata hivyo, Kanisa Katoliki limetumia kila njia iwezekanayo ili kudumisha udhibiti imara wa watu. Kwa kuwakaza maofisa wa serikali, walihakikisha kwamba wamishonari Mashahidi waliamriwa waondoke Italia mwaka 1949 na kwamba, ilipowezekana, ruhusa zilizopatikana na Mashahidi kwa ajili ya makusanyiko huko zilifutwa wakati wa miaka ya 1950.

  • “Vitu vya Kuchukiwa na Mataifa Yote”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Katika Jamhuri ya Dominika, makasisi walishirikiana na Dikteta Trujillo, wakimtumia ili kutimiza malengo yao kwa jinsi ileile aliyowatumia kutimiza makusudi yake. Katika 1950, baada ya makala za magazeti zilizoandikwa na mapadri kuwashutumu Mashahidi wa Yehova, mwangalizi wa tawi la Watch Tower Society aliitwa na Katibu wa Mambo ya Ndani na Polisi. Alipokuwa akingoja nje ya ofisi, mwangalizi wa tawi aliona mapadri wawili Wayesuiti wakiingia na kisha kuondoka. Mara tu baada ya hiyo, aliitwa ndani katika ofisi ya yule Katibu, na huyo Katibu akasoma kwa wasiwasi sheria iliyopiga marufuku utendaji wa Mashahidi wa Yehova. Baada ya marufuku kuondolewa kifupi katika 1956, makasisi walitumia redio na magazeti pia katika uchongezi mpya dhidi ya Mashahidi. Makutaniko mazimamazima yalikamatwa na kuagizwa kutia sahihi taarifa ya kukana imani yao na kuahidi kurudi kwenye Kanisa la Katoliki ya Roma. Mashahidi walipokataa, walipigwa, wakapigwa kwa mateke, wakapigwa kwa viboko, na nyuso zao zikapondwa kwa ma­tako ya bunduki. Lakini walisimama imara, na idadi zao zikaongezeka.

  • “Vitu vya Kuchukiwa na Mataifa Yote”
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Katika baadhi ya nchi za Afrika, wamejaribu kuwavuta maofisa wawafukuze Mashahidi wa Yehova kutoka nchi hizo au kuwanyima uhuru wa kuzungumza juu ya Neno la Mungu kwa wengine. Ingawa huenda makasisi Wakatoliki na Waprotestanti wakatofautiana katika mambo mengine, wao wanakubaliana katika kuwapinga Mashahidi wa Yehova. Pindi nyingine hata wameungana pamoja ili kujaribu kuvuta maofisa wa serikali wakomeshe utendaji wa Mashahidi. Mahali ambako dini zisizo za Kikristo ndizo zimemiliki maisha, mara nyingi wao pia wametumia serikali ili kuzuia watu wao wasipate kujua mafundisho yanayoweza kuwafanya waulize maswali juu ya dini za uzawa wao.

      Nyakati nyingine, vikundi hivyo visivyo vya Kikristo vimeungana na wale wanaodai kuwa Wakristo katika kupanga kudumisha hali ya kidini iliyoko. Katika Dekin, nchini Dahomey (sasa Benin), mganga mmoja mkuu na padri Mkatoliki walishauriana pamoja kuwafanya maofisa wakandamize utendaji wa Mashahidi wa Yehova mapema katika miaka ya 1950. Katika jitihada zao walitunga mashtaka bandia yaliyokusudiwa kuzusha aina zote za hisiamoyo za uhasama. Walishtaki kwamba Mashahidi walikuwa wakiwahimiza watu waasi dhidi ya serikali, hawakuwa wakilipa kodi, walisababisha waganga wasilete mvua, na walisababisha kule kukosa kufanikiwa kwa maombi ya padri.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki