-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
Barua moja ya uchungaji iliyotolewa na maaskofu wa Ukatoliki wa Ujeremani katika Septemba 1939 ilipotokea Vita ya Ulimwengu 2, inatoa nuru juu ya jambo hili. Kwa sehemu inasomwa hivi: “Katika saa hii ya kukata maneno sisi twashauri askari-jeshi Wakatoliki kufanya wajibu wao katika utii kwa Fuehrer na kuwa tayari kudhabihu nafsi nzima yao. Sisi tunasihi Waaminifu wajiunge katika sala zenye idili kwamba huu Mwongozo wa Kimungu uweze kupeleka vita hii kwenye ufanisi wenye baraka.”
-
-
Kuhukumu Kahaba Mwenye Sifa MbayaUfunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 238]
Chini ya kichwa hiki, makala inayofuata ilitokea katika chapa ya kwanza ya The New York Times ya Desemba 7, 1941:
‘SALA YA VITA’ KWA AJILI YA REICH
Maaskofu wa Kikatoliki katika Fulda Waomba Baraka na Ushindi
Kongamano la Maaskofu wa Kikatoliki wa Ujeremani lililokusanyika katika Fulda limependekeza ianzishwe ‘sala ya vita’ maalumu ambayo itasomwa mwanzoni na mwishoni mwa ibada zote za kimungu. Sala hiyo husihi Mungu abariki silaha za Ujeremani kwa ushindi na kutoa himaya kwa maisha na afya ya askari-jeshi wote. Maaskofu hao waliwaagiza zaidi makasisi wa Kikatoliki waweke na kukumbuka katika mahubiri maalumu ya Jumapili angalau mara moja kwa mwezi askari-jeshi Wajeremani ‘barani, baharini na hewani.’”
Makala hii iliondolewa kwenye chapa za baadaye za nyusipepa hiyo. Desemba 7, 1941, ndiyo siku Japani, nchi fungamani na Ujeremani, iliposhambulia meli za U.S. kwenye Pearl Harbor.
[Picha katika ukurasa wa 244]
“Majina ya Kufuru”
Hayawani-mwitu mwenye pembe mbili alipoendeleza Ushirika wa Mataifa baada ya Vita ya Ulimwengu 1, hawara zake wa kidini walitafuta mara hiyo kulipa tendo hilo idhini ya kidini. Kama tokeo, tengenezo jipya la amani ‘likajawa na majina ya kufuru.’
-