Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maisha Katika Nyakati za Biblia—Pesa
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Mei 1
    • Jinsi Sarafu Zilivyotengenezwa Mara ya Kwanza

      Yaelekea sarafu za kwanza zilitengenezwa huko Lidia (Uturuki ya kisasa), wakati fulani kabla ya mwaka wa 700 K.W.K. Muda mfupi baadaye, wafanyakazi wa vyuma kutoka nchi mbalimbali walianza kutengeneza sarafu kwa wingi, na watu katika nchi zote zinazotajwa katika Biblia wakaanza kuzitumia.

      Ni Mbinu gani iliyotumiwa kutengeneza sarafu? Mfanyakazi wa vyuma angetoa chuma kilichoyeyushwa kutoka motoni (1) na kumwaga myeyuko huo ndani ya kifaa chenye vishimo vidogo na kutokeza sarafu za mviringo zisizo na maandishi (2). Kisha angeweka sarafu hizo katikati ya vyuma viwili vya kupigia chapa ambavyo vilikuwa na alama fulani au picha (3). Halafu angegonga vyuma hivyo kwa nyundo na alama au picha ingetokea kwenye sarafu (4). Kwa sababu kazi hiyo ilifanywa haraka-haraka, mara kwa mara picha au alama hizo hazikutokea katikati ya sarafu. Wafanyakazi hao wangetenganisha sarafu hizo na kupima uzito wake ili kuhakikisha zilikuwa na uzito uleule, na ikiwa zilihitaji kuchongwa, walifanywa hivyo (5).

  • Maisha Katika Nyakati za Biblia—Pesa
    Mnara wa Mlinzi—2011 | Mei 1
    • [Sanduku/​Picha katika ukurasa wa 26]

      Habari Kuhusu Sarafu Mbalimbali

      ● Mojawapo ya sarafu ndogo zaidi iliyotumiwa Palestina katika karne ya kwanza ni leptoni ya shaba, ambayo pia iliitwa sarafu ndogo. Mfanyakazi angelipwa leptoni mbili kwa kazi ya dakika 15 tu. Yaelekea yule mjane aliweka leptoni mbili katika sanduku la mchango la hekaluni.—Marko 12:42.

      ● Drakma ya fedha ilikuwa sarafu ya Wagiriki ambayo mfanyakazi alilipwa baada ya kazi ya siku nzima. (Luka 15:8, 9) Wanaume wote Wayahudi walilipa drakma mbili kila mwaka kama kodi ya hekalu.—Mathayo 17:24.

      ● Dinari ya fedha ilikuwa sarafu ya Waroma iliyokuwa na picha ya Kaisari, hivyo ilifaa sana kutumiwa kama sarafu ya “ushuru” ambao ulitolewa na kila kijana Myahudi wakati wa utawala wa Waroma. (Waroma 13:7) Mwajiri angemlipa mfanyakazi wake dinari moja kwa kufanya kazi saa 12 kwa siku.—Mathayo 20:2-14.

      ● Shekeli ya fedha kutoka jiji la Tiro iliyotengenezwa kwa madini ya fedha halisi, ilikuwa ikitumiwa huko Palestina wakati Yesu alipokuwa duniani. Yaelekea “vipande 30 vya fedha” ambavyo wakuu wa makuhani walimlipa Yuda Iskariote ili amsaliti Yesu vilikuwa shekeli za Tiro.—Mathayo 26:14-16.

      Sarafu katika ukubwa halisi

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki