-
Sehemu ya 4—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
Harold na Anne Zimmerman walikuwa miongoni mwa wale waliohama. Walikuwa tayari wametumikia wakiwa walimu wamishonari katika Ethiopia. Hata hivyo, katika 1959, wakati walipokuwa wakikamilisha mipango ya kuhama kutoka Marekani kwenda Kolombia kushiriki katika kueneza ujumbe wa Ufalme huko, walikuwa wakilea watoto wanne, waliokuwa na umri wa kuanzia miezi mitano hadi miaka mitano. Harold alitangulia ili kutafuta kazi. Wakati alipowasili nchini, matangazo ya habari nchini yalimtia wasiwasi. Vita isiyo rasmi ya wenyewe kwa wenyewe ilikuwa ikiendelea, na kulikuwa mauaji mengi katika sehemu za mashambani za nchi. ‘Je, kweli mimi nataka kuleta familia yangu iishi katika hali kama hizi?’ akajiuliza. Alijaribu kukumbuka kielelezo cha kumwongoza au kanuni ya Biblia. Jambo lililokuja akilini mwake ni lile simulizi la Biblia la wapelelezi wenye woga waliorudisha kwenye kambi ya Waisraeli ripoti mbaya kuhusu Bara la Ahadi. (Hes. 13:25–14:4, 11) Jambo hilo lilimwezesha kufikia uamuzi; yeye hakutaka kuwa kama wao! Mara moja akapanga familia yake ije. Ilikuwa ni mpaka pesa zao zilipopungua kufikia dola tatu tu ndipo alipopata kazi ya kimwili aliyohitaji, lakini walikuwa na vitu vya lazima kabisa. Kiasi cha kazi aliyolazimika kufanya ili kuruzuku familia yake kilibadilika kadiri miaka ilivyopita, lakini sikuzote yeye amejitahidi kutanguliza masilahi ya Ufalme. Walipokwenda Kolombia kwanza, kulikuwa Mashahidi kama 1,400 nchini. Lo! ni ukuzi wa kustaajabisha kama nini ambao wameona tangu hapo!
-
-
Sehemu ya 4—Kuwa Mashahidi Hadi Sehemu ya Mbali Zaidi Sana ya DuniaMashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
-
-
[Picha katika ukurasa wa 469]
Miongoni mwa maelfu ya Mashahidi waliohamia nchi nyinginezo kutumikia sehemu ambako uhitaji ulikuwa mkubwa zaidi walikuwa familia, kama vile Harold na Anne Zimmerman pamoja na watoto wao wanne wachanga (Kolombia)
-