Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Usitawi wa Muundo wa Tengenezo
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Wanaume na wanawake ambao hawakuwa na familia zilizowategemea na ambao wangeweza kutoa kabisa nusu au zaidi ya wakati wao kwa kazi ya Bwana walitiwa moyo waanze kazi wakiwa waeneza-evanjeli makolpota. Idadi hiyo ilitofautiana sana mwaka mmoja na mwingine, lakini kufikia 1885 kulikuwa tayari kama 300 waliokuwa wakishiriki kazi hiyo wakiwa makolpota. Baadhi yao pia walishiriki lakini kwa kadiri ndogo zaidi. Madokezo yalitolewa kwa makolpota kuhusu jinsi ya kufanya kazi yao. Lakini shamba lilikuwa kubwa, na angalau mwanzoni, waliteua eneo lao wenyewe na kwenda toka eneo moja hadi jingine sanasana kama walivyoona kuwa vema. Halafu walipokutana kwenye mikusanyiko, walikuwa wakifanya marekebisho yaliyohitajiwa ili kuratibu jitihada zao.

  • Usitawi wa Muundo wa Tengenezo
    Mashahidi wa Yehova—Wapiga-Mbiu wa Ufalme wa Mungu
    • Toleo la Machi 1, 1917, la The Watch Tower lilitangaza kwamba, kuanzia hapo na kuendelea, ofisi ya Sosaiti itakuwa ikiwagawia makolpota na wafanyakazi wa uchungajie katika makutaniko maeneo yote ya kufanyia kazi. Mahali palipokuwa na wafanyakazi wenyeji na makolpota pia wakishiriki katika utumishi kama huo wa shambani katika jiji au wilaya, eneo liligawanywa miongoni mwao na halmashauri ya wilaya ya mahali iliyowekwa.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki