Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kushinda Udhaifu wa Kibinadamu
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Machi 15
    • 4. Paulo alitoa ushauri gani kwenye 1 Wakorintho 10:12, 13?

      4 Paulo alipowaandikia Wakristo walioishi Korintho—jiji lililojulikana kwa upotovu wake wa maadili—alitoa onyo la busara dhidi ya kishawishi na nguvu ya dhambi. Alisema: “Acheni yeye ambaye afikiri kuwa amesimama ajihadhari kwamba asianguke.

  • Kushinda Udhaifu wa Kibinadamu
    Mnara wa Mlinzi—2001 | Machi 15
    • Usijitumaini Kupita Kiasi

      5. Kwa nini ni hatari kujitumaini kupita kiasi?

      5 Paulo asema: “Acheni yeye ambaye afikiri kuwa amesimama ajihadhari kwamba asianguke.” Ni hatari kutumaini kupita kiasi nguvu zetu za kiadili. Hilo laonyesha hatuelewi hali na nguvu ya dhambi. Kwa kuwa watu kama Musa, Daudi, Solomoni na mtume Petro walifanya dhambi, je, tuhisi kwamba sisi tu salama? (Hesabu 20:2-13; 2 Samweli 11:1-27; 1 Wafalme 11:1-6; Mathayo 26:69-75) “Mwenye hekima huogopa, akajitenga na uovu; bali mpumbavu ana ufidhuli, na kujitumai,” lasema andiko la Mithali 14:16. Isitoshe, Yesu alisema: “Roho ni yenye hamu, lakini mwili ni dhaifu.” (Mathayo 26:41) Kwa kuwa hakuna mwanadamu asiye mkamilifu ambaye hawezi kudhuriwa na tamaa zilizopotoka, twahitaji kuchukua onyo la Paulo kwa uzito na kukinza kishawishi, la sivyo tutakuwa katika hatari ya kuanguka.—Yeremia 17:9.

      6. Yatupasa kujitayarisha lini na jinsi gani kwa ajili ya kishawishi?

      6 Ni jambo la hekima kujitayarisha kwa matatizo ambayo huenda yakatokea bila kutarajiwa. Mfalme Asa alitambua kwamba kipindi cha amani ndio wakati uliofaa kwake kuimarisha ulinzi wake. (2 Mambo ya Nyakati 14:2, 6, 7) Alijua kwamba ingekuwa kuchelewa mno kujitayarisha wakati wa shambulio. Vivyo hivyo, maamuzi kuhusu yale tupaswayo kufanya vishawishi vinapotokea hufanywa vizuri zaidi wakati akili imetulia na mazingira ni yenye amani. (Zaburi 63:6) Danieli na marafiki wake wenye kumhofu Mungu walifanya uamuzi wao wa kuwa waaminifu kwa sheria ya Yehova kabla hawajashinikizwa kula vyakula vitamu vya mfalme. Hivyo, walishikilia imani yao, wakakataa kula chakula kisicho safi. (Danieli 1:8) Kabla hali zenye kushawishi hazijatokea, acheni tuimarishe azimio letu la kudumu tukiwa safi kiadili. Ndipo tutakapoweza kukinza dhambi.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki