Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Kufungua Kufuli ya Siri Takatifu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Watu wowote waliopinga mafundisho au mamlaka ya kanisa walikandamizwa bila rehema, na maelfu yasiyohesabika ya wale walioitwa eti wazushi wa kidini waliteswa-teswa mpaka kifo au wakachomwa penye nguzo. Hivyo Shetani alijitahidi kuhakikisha kwamba mbegu yoyote ya kweli ya tengenezo la Yehova lililo mfano wa mwanamke ingepondwa-pondwa kwa haraka sana.

  • Kufungua Kufuli ya Siri Takatifu
    Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
    • Ile Mbegu Yavumilia

      17. (a) Fumbo la maneno la Yesu la ngano na magugu lilitabiri nini? (b) Ni jambo gani lililotukia katika 1918, likitokeza kukataliwa gani na kuwekwa rasmi gani?

      17 Katika fumbo lake la maneno la ngano na magugu, Yesu alitabiri ule wakati wa giza ambao ungekuwako wakati Jumuiya ya Wakristo ilitawala ikiwa na mamlaka yote. Hata hivyo, kupitia karne zote za uasi-imani, kungekuwako Wakristo mmoja mmoja wa mfano wa ngano, wapakwa-mafuta halisi. (Mathayo 13:24-29, 36-43) Hivyo, wakati siku ya Bwana ilipopambazuka katika Oktoba 1914, Wakristo wa kweli walikuwa wangali wapo duniani. (Ufunuo 1:10) Inaonekana kwamba Yehova alikuja kwenye hekalu lake la kiroho kwa ajili ya kuhukumu karibu miaka mitatu na nusu baadaye, katika 1918, akiandamana na Yesu akiwa “mjumbe wa agano” wake. (Malaki 3:1; Mathayo 13:47-50) Ulikuwa wakati wa kukataa hatimaye wale Wakristo bandia na kuweka rasmi ‘yule mtumwa mwaminifu na mwenye akili juu ya mali yake yote.’—Mathayo 7:22, 23; 24:45-47.

      18. Ni “saa” ipi iliyokuja katika 1914, nao ulikuwa wakati wa yule mtumwa kufanya nini?

      18 Pia ulikuwa wakati wa mtumwa huyu kutoa uangalifu wa pekee kwa vile vitu vilivyoandikwa katika zile jumbe za Yesu zilizopelekwa kwa makundi saba, kama tunavyoona kutokana na mambo yaliyotaarifiwa humo. Mathalani, Yesu anarejeza kwenye kuja kwake kuhukumu makundi, hukumu ambayo ilianza katika 1918. (Ufunuo 2: 5, 16, 22, 23; 3:3) Yeye anasema juu ya kulipa himaya kundi la Filadelfia juu ya “ile saa ya mtihani ambayo yapasa ije juu ya dunia yote nzima inayokaliwa.” (Ufunuo 3:10, 11, NW) Hii “saa ya mtihani” inawasili inapopambazuka tu siku ya Bwana katika 1914, ambayo baada ya hiyo Wakristo walitahiniwa kwa habari ya ushikamanifu wao kwa Ufalme wa Mungu uliosimamishwa.—Linga Mathayo 24:3, 9-13.

      19. (a) Yale makundi saba yanafananisha nini leo? (b) Ni nani ambao wameshirikiana na Wakristo wapakwa-mafuta wakiwa hesabu kubwa-kubwa na kwa nini lile shauri la Yesu na hali anazoeleza Yesu huhusu wao pia? (c) Imetupasa sisi tuzioneje zile jumbe za Yesu kwa yale makundi saba ya karne ya kwanza?

      19 Kwa sababu hii, maneno ya Yesu kwa yale makundi yamekuwa na utumizi wayo mkubwa tangu 1914. Katika mazingira haya, yale makundi saba yanafananisha makundi yote ya Wakristo wapakwa-mafuta katika kipindi cha hii siku ya Bwana.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki