Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Fahari Iliyosahaulika ya Milki ya Byzantium
    Amkeni!—2001 | Oktoba 8
    • Hata hivyo, wengi wanakubali kwamba Milki ya Byzantium ilianza kuwa maarufu wakati Mfalme Konstantino alipohamisha jiji kuu la milki yake kutoka Roma hadi Byzantium mwaka wa 330 W.K. Aliliita jiji hilo Constantinople (leo ni Istanbul), kutokana na jina lake.

  • Fahari Iliyosahaulika ya Milki ya Byzantium
    Amkeni!—2001 | Oktoba 8
    • Jiji Kuu Lenye Fahari

      Mwanahistoria mmoja anasema Constantinople la kale lilikuwa jiji “maarufu sana lenye ufanisi.” Jiji la Constantinople lililokuwa kati ya Ulaya na Asia—katika Mlango-Bahari wa Bosporus—lilizingira rasi salama na bandari yenye ulinzi, iliyoitwa Golden Horn. Katika mwaka wa 657 K.W.K., walowezi Wagiriki waliliita jiji hilo Byzantium kutokana na jina la kiongozi wao mashuhuri Byzas. Baada ya karne kumi kupita, jiji hilo lilionwa kuwa Roma Mpya. Lilikuwa na wakazi wapatao nusu milioni lilipofikia kilele cha ustawi kati ya karne ya 6 na ya 11 W.K.

      Watalii kutoka nchi za Magharibi walistaajabia jiji hilo kuu lililokuwa kituo muhimu cha kibiashara ulimwenguni. Bandari yake ilijaa mashua. Hariri, manyoya ya wanyama, johari, mbao zenye uturi, pembe za ndovu zilizochongwa, dhahabu, fedha, vito vilivyopakwa enameli, na vikolezo viliuzwa masokoni. Ndiyo sababu jiji la Constantinople lilionewa wivu na mataifa mengine yenye nguvu hivi kwamba yalijaribu tena na tena kulivamia. Kabla ya kushindwa na Uturuki mwaka wa 1453, maadui walifaulu kuvamia jiji hilo mara moja tu—yaani, “Wakristo” wa Krusedi ya Nne. Mpiganaji wa kidini Robert wa kutoka Clari alisema kwa mshangao kwamba “tangu ulimwengu kuumbwa hazina kubwa hivyo haijawahi kuwapo kamwe wala kupatikana.”

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki