-
Mambo Ambayo Wengine WamesemaAmkeni!—2010 | Agosti
-
-
Italia “Watu 30,000 wamekaa kimya katika Uwanja wa Michezo wa Olympic . . . Hakuna takataka zinazotupwa ovyoovyo, hakuna kelele. Hivyo ndivyo hali ilivyokuwa jana katika Uwanja wa Michezo wa Olympic . . . Hakuna mtu anayetoa ishara za matusi, hakuna sigara au hata mikebe [ya vinywaji] iliyotupwa ovyoovyo. Watu walikuwa wamefungua Biblia, wakinukuu mambo makuu, na watoto wakiwa wamekaa kimya.”—Gazeti L’Unità, likiripoti kuhusu kusanyiko la Mashahidi wa Yehova huko Rome.
-
-
Mambo Ambayo Wengine WamesemaAmkeni!—2010 | Agosti
-
-
Brazili Gazeti moja liliripoti hivi: “Mashahidi wa Yehova hufanya mambo kwa njia inayopendeza sana. Mahali wanapokutania huwa safi kila mara. Kila kitu huwa kimepangwa vizuri . . . Wanapomaliza shughuli zao, wao huacha mahali hapo pakiwa safi kuliko palivyokuwa. Hotuba zinapoendelea mahali hapo huwa kimya. Hawasukumani wala kugongana. Wao huwa na tabia nzuri wakati wote. . . . Kwa kweli hii ni dini yenye utaratibu. Wanajua jinsi Mungu anavyopaswa kuabudiwa.”—Gazeti Comércio da Franca.
-