Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Matumbawe—Yamo Hatarini na Yanakufa
    Amkeni!—1996 | Septemba 22
    • Tumbawe lenye afya ni lenye rangi ya kikahawia, kijani kibichi, nyekundu, au kimanjano, ikitegemea aina ya miani inayoishi katika vichaza wa tumbawe wenye miili yenye kupenyezwa na nuru. Miani isiyoweza kuonekana kwa macho hutumia nuru inayoangaza kupitia wenzi wayo wanyama na kufyonza taka za vichaza, kutia ndani kaboni dioksidi, kwa ajili ya lishe yayo. Kupitia usanidimwanga, nayo miani huandalia tishu za tumbawe oksijeni, chakula, na nishati. Ushirikiano huo pamoja na miani huruhusu tumbawe likue haraka zaidi na kuendelea kuishi katika maji ya tropiki yasiyo na lishe. Miani na tumbawe hufurahia zaidi ubora wa ulimwengu wa mimea na wanyama. Ni ubuni stadi na wenye hekima kama nini!

  • Matumbawe—Yamo Hatarini na Yanakufa
    Amkeni!—1996 | Septemba 22
    • Lishe ya tumbawe huandaliwa na miani (iitwayo kwa kisayansi zooxanthellae), ambayo huishi katika mwili wenye kupenyezwa na nuru wa vichaza, na pia na wanyama wasioweza kuonekana kwa macho ambao hushikwa na mikono ya tumbawe. Matokeo ni mwamba wa matumbawe ambao ni makao ya maelfu ya spishi za viumbe vya bahari katika bahari-kuu isiyo na kinga.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki