-
Abrolhos—Inavutia MachoAmkeni!—2002 | Desemba 22
-
-
Abrolhos—Inavutia Macho
NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI BRAZILI
KATIKA karne ya 16, mabaharia waliokuwa karibu na pwani ya jimbo la Bahia huko Brazili, waliwatahadharisha mabaharia wenzao kuhusu miamba ya matumbawe iliyokuwa karibu kwa kusema: “Abra os olhos!” (Kaeni Macho!) Kulingana na masimulizi, visiwa vitano vidogo katika eneo hilo viliitwa Abrolhos kutokana na tahadhari hiyo iliyorudiwa mara nyingi.
Visiwa vya Abrolhos viko Kusini mwa Bahari ya Atlantiki, kilometa 80 tu kutoka kwenye miji ya pwani ya Caravelas na Alcobaça. Hata hivyo, eneo hilo limezungukwa na kutenganishwa na miamba ya matumbawe. Kama yule nyangumi mwenye nundu hangepatikana huko, mabaharia wengi hawangethubutu kufika kwenye eneo hilo ambalo lina miamba ya matumbawe iliyofichika na ambalo hukumbwa na dhoruba kali. Nyangumi huyo ana faida kubwa kiuchumi.
-
-
Abrolhos—Inavutia MachoAmkeni!—2002 | Desemba 22
-
-
Miamba ya Matumbawe Yaliyo Kama Kuta na Kofia
“Nahodha wetu Manoel alipokuwa akiiongoza mashua kati ya miamba ya matumbawe inayoitwa Kuta za Miamba ya Matumbawe, nilielewa kile kilichowafanya mabaharia Wareno waogope eneo hilo. Nguzo za matumbawe yenye rangi mbalimbali zilitokeza juu ya maji. Nguzo hizo zina urefu wa meta 20 na upana wa meta 50 karibu na uso wa maji. Kwa kuwa miamba hiyo ya matumbawe ina umbo la uyoga, wenyeji wa eneo hilo wameiita kofia kubwa. Nguzo nyingi chini ya maji zimeshikamana na kuwa matao makubwa na vijia na hata kuta zenye urefu wa kilometa 20 ambazo zinatokeza juu ya maji kama majukwaa ya miamba. Hizo ndizo zinazoitwa Kuta za Miamba ya Matumbawe.
-