-
Korintho “Jiji Linalomiliki Bandari Mbili”Mnara wa Mlinzi—2009 | Machi 1
-
-
Mashua ndogo zilivutwa kuvuka shingo hiyo ya nchi kupitia njia iliyoitwa diolkos.—Ona sanduku kwenye ukurasa wa 27.
-
-
Korintho “Jiji Linalomiliki Bandari Mbili”Mnara wa Mlinzi—2009 | Machi 1
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 27]
DIOLKOS—NJIA YA KUPITISHIA MELI NCHI KAVU
Kufikia mwishoni mwa karne ya saba K.W.K., mipango ya kujenga mfereji iliposhindwa kufaulu, Periander, mtawala wa Korintho, alijenga njia ya kusafirisha meli kuvuka shingo hiyo ya nchi kwa ustadi mwingi.a Njia hiyo iliyoitwa diolkos, jina linalomaanisha “kokota-ng’ambo,” ilikuwa njia yenye mawe ya mraba na mbao zilizowekwa kwenye nafasi zilizoachwa na mawe hayo ambazo zilikuwa zimepakwa mafuta. Mizigo kutoka kwa meli zilizotia nanga katika bandari moja ilipakuliwa, ikatiwa juu ya mikokoteni yenye magurudumu, na kuvutwa na watumwa juu ya njia hiyo na kupelekwa upande ule mwingine. Meli ndogo ambazo nyakati nyingine zilikuwa na mizigo zilivutwa kupitia njia hiyo.
[Maelezo ya chini]
a Ili kupata habari kuhusu historia ya ujenzi wa mfereji wa kisasa, ona makala yenye kichwa “The Corinth Canal and its Story,” katika Amkeni! la Desemba 22, 1984, ukurasa wa 25-27 la Kiingereza au Amkeni! la Machi 22, 1985 la Kifaransa.
-