-
Korintho “Jiji Linalomiliki Bandari Mbili”Mnara wa Mlinzi—2009 | Machi 1
-
-
Kwenye Barabara ya Lechaeum ambayo ilikingwa na kuta mbili, kulikuwa na njia za wapita-njia, majengo ya serikali, mahekalu, na maduka. Huenda Paulo alikutana na wanunuzi wenye shughuli nyingi, watu waliosimama kupiga gumzo, wenye maduka, watumwa, wafanyabiashara, na wengine—watu ambao aliwahubiria.
-
-
Korintho “Jiji Linalomiliki Bandari Mbili”Mnara wa Mlinzi—2009 | Machi 1
-
-
Huenda shughuli za meli za kibiashara katika bandari hiyo zilichangia katika kumfanya mtume Paulo afanye kazi ya kutengeneza hema huko Korintho. (Matendo 18:1-3) Kitabu kimoja (In the Steps of St. Paul) kinasema hivi: “Majira ya baridi kali yalipokaribia, watengenezaji hema wa Korintho ambao pia walitengeneza matanga, walikuwa na kazi nyingi kupita kiasi. Kwa kuwa bandari zote mbili zilijaa meli zilizokuwa zikijikinga majira hayo na mabaharia wakijitahidi kurekebisha meli zao wakati huo, kila mtu katika Lechæum na Kenkrea ambaye angeweza kushona matanga hata kwa kiasi kidogo alipewa kazi hiyo.”
Baada ya kukaa Korintho kwa zaidi ya miezi 18, Paulo alisafiri kutoka Kenkrea hadi Efeso katika mwaka wa 52 W.K. hivi. (Matendo 18:18, 19)
-
-
Korintho “Jiji Linalomiliki Bandari Mbili”Mnara wa Mlinzi—2009 | Machi 1
-
-
Hata hivyo, kulikuwa na faida kwa sababu ya kuwa na mchanganyiko huo wa watu wa mataifa mbalimbali. Jiji hilo lilipata mawazo mapya kila wakati. Wakaaji wake walikuwa na akili zilizofunguka zaidi kuliko watu wa majiji mengine ambayo Paulo alitembelea. “Watu kutoka mashariki na magharibi walikutana katika jiji hilo la kale lenye bandari,” akasema mchanganuzi mmoja wa Biblia, “na hivyo kuwafanya wakaaji wake wapate mawazo, falsafa, na dini za kila aina ulimwenguni.” Kwa sababu hiyo, kulikuwa na dini tofauti-tofauti na hilo lilirahisisha kazi ya Paulo ya kuhubiri.
-