Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Ganda la Mti Linalofanyiza Kifuniko cha Chupa
    Amkeni!—2011 | Julai
    • KIZIBO au kifuniko kinachotumiwa hasa kufunika chupa za mvinyo kimetolewa kwenye aina fulani ya mti wa mwaloni. Lakini ganda lake si la kawaida. Ni jepesi, halishiki moto, na linaweza kutanuka.

      Kila mwaka, mti huo wa mwaloni huongeza sana ukubwa wa ganda lake. Iwapo ganda lake halitavunwa, linaweza kukua kufikia unene wa sentimita 25—nalo husaidia mti huo usipigwe na jua, baridi, wala na moto wa msitu. Ganda lake linapovunwa, mti huo wa mwaloni utakuza ganda lingine katika muda wa miaka kumi hivi.

  • Ganda la Mti Linalofanyiza Kifuniko cha Chupa
    Amkeni!—2011 | Julai
    • Haiharibu Mazingira

      Msitu mzuri wa aina hii ya mialoni unaonyesha wazi kwamba mwanadamu anaweza kuishi kwa upatano na mazingira—akifaidika kutokana na mazao yake bila kuharibu utajiri wake. Mialoni hiyo ya kale hurembesha maeneo ya vijijini, huandaa kivuli na chakula kwa ajili ya mifugo inayolisha chini yake, na kupunguza ukali wa majira ya kiangazi.

      Ndege kadhaa ambao wanakabili hatari ya kutoweka—kutia ndani tai anayeitwa imperial, tumbusi mweusi, na korongo mweusi—hupendelea hasa kujenga viota vyao juu ya mialoni mikubwa. Pia, simba-mangu wa Iberia ambaye anakabili hatari ya kutoweka anaishi katika misitu hiyo ya mialoni. Hivi karibuni, Hazina ya Wanyama wa Pori Ulimwenguni ilisema kwamba kuokoka kwa mnyama huyo kunategemea biashara ya ganda hilo la mwaloni nchini Hispania na Ureno.

  • Ganda la Mti Linalofanyiza Kifuniko cha Chupa
    Amkeni!—2011 | Julai
    • a Aina hii ya mti wa mwaloni unapatikana katika sehemu nyingine za ulimwengu, lakini eneo la Mediterania ndilo hutokeza vifuniko au vizibo vyake kwa ajili ya biashara, kwa kuwa mti huo hukua kwa njia ya asili katika eneo hilo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki