-
Fahari ya OkidiAmkeni!—2003 | Septemba 8
-
-
Fahari ya Okidi
NA MWANDISHI WA AMKENI! NCHINI KOSTA RIKA
“Huonyesha urembo wake kwenye ukuta wenye vigae. Hupepea-pepea kwenye upepo. Na kivuli, na jua, huyafanya yapendeze zaidi, na sasa kuliko wakati mwingine wowote, yana fahari zaidi.”
HUO ulikuwa utangulizi wa makala moja ya gazeti iliyokuwa ikitangaza Maonyesho ya Okidi ya Kitaifa ya Kila Mwaka huko San José, Kosta Rika. Kutajwa tu kwa jina okidi kwaweza kumfanya mtu akumbuke baadhi ya maua maridadi sana ulimwenguni. Mgeni aliyehudhuria maonyesho hayo alisikika akisema: “Baada ya kutazama uzuri huo wa ajabu, ni nani anayeweza kukana kwamba Mungu ndiye aliyeyaumba?”
-
-
Fahari ya OkidiAmkeni!—2003 | Septemba 8
-
-
Okidi za Kosta Rika
Kosta Rika ni nchi ndogo lakini ina mojawapo ya idadi kubwa zaidi ya okidi ulimwenguni. Ama kweli, nchi hiyo ina jamii zipatazo 1,400 tofauti-tofauti, na nyingine bado hazijagunduliwa. Kosta Rika ni eneo lenye hali zinazobadilika-badilika za unyevu na hivyo linafaa kwa ukuzi wa okidi mbalimbali kwa sababu ya hali nzuri ya hewa inayosababishwa na Bahari ya Karibea upande wa Mashariki na Bahari ya Pasifiki upande wa Magharibi. Pia katika nchi hiyo kuna misitu mingi ya mvua ambamo okidi nyingi husitawi. Mti wenye aina 47 za okidi ulipatikana katika msitu mmoja wa mvua!
Jitihada zaendelea kufanywa ili kuokoa jamii nyingi za okidi ambazo ziko hatarini. Ingawa hivyo, inafurahisha kwamba jamii nyingine bado husitawi katika misitu ya Kosta Rika. Leo, watu wa aina zote wanapenda kukuza okidi. Si vigumu kukuza okidi, lakini kuna tatizo moja. Si rahisi kuacha kukuza okidi ukisha zoea. Mwandishi mmoja aliandika hivi: “Kuwa na okidi moja ni kama kujaribu kula njugu moja tu!”
-
-
Fahari ya OkidiAmkeni!—2003 | Septemba 8
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 23]
Maonyesho ya Okidi ya Kitaifa ya Kila Mwaka
Chama cha Wakuzaji wa Okidi nchini Kosta Rika kilipanga maonyesho ya kitaifa ya kwanza katika mwaka wa 1971 ili kuwajulisha watu wengi zaidi uhitaji wa kuhifadhi mazingira ya asili ya okidi. Maonyesho ya kwanza yalikuwa madogo yakiwa na mimea 147 kwenye meza chache. Hata hivyo, mwaka mmoja hivi karibuni mimea zaidi ya 1,600 ilionyeshwa. Wanapofika kwenye maonyesho hayo, wageni huona rangi mbalimbali wanapotazama okidi za ukubwa na maumbo mbalimbali.
[Hisani]
Jardín Botánico Lankester
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 24]
Bustani ya Lankester
Bustani hii tulivu iliyoanzishwa mwaka wa 1917 na mtaalamu wa viumbe Charles Lankester Wells kutoka Uingereza, huonwa kuwa mojawapo ya bustani zenye thamani zaidi huko Amerika. Bustani ya Lankester ina jamii 800 za okidi za kienyeji na za kutoka nchi nyingine zinazokua katika eneo la ekari 26 lenye msitu na mbuga. Pia hutumiwa kama hifadhi ya kitaifa. Nyakati nyingine okidi-mwitu—hasa zile zilizo adimu—huuzwa kimagendo. Wenye mamlaka wanapozipata okidi hizo, wanazileta kwenye Bustani ya Lankester ili kuzihifadhi.
[Hisani]
Photos above: Jardín Botánico Lankester de la Universidad de Costa Rica
-