Amkeni!—“Chombo Muhimu Chenye Thamani Sana”
“ASANTENI kwa makala yenu iliyokuwa na kichwa ‘RSD—Ugonjwa wa Kukoroweza na Wenye Maumivu,’ katika toleo la Septemba 8, 1997. Nikiwa ripota wa mambo ya mahakamani, mara nyingi mimi huitwa kurekodi ushuhuda juu ya masuala mengi ya namna mbalimbali na yaliyo tata. Hivi majuzi niliripoti taarifa ya mtaalamu wa nusukaputi anayeshughulikia kudhibiti maumivu. Mada ya habari nzima ya ushuhuda ilikuwa RSD [Reflex Sympathetic Dystrophy]. Kwa sababu ya kusoma Amkeni! kwa ukawaida, mara moja nilifahamu ugonjwa huo na njia za matibabu, ambazo zote zilielezwa waziwazi katika toleo hilo la Septemba. Baadaye niliweza kushiriki makala hii na baadhi ya mawakili waliohusika katika kesi hiyo.
“Naliona Amkeni! kuwa chombo muhimu chenye thamani sana kinachoendelea kunifundisha. Amkeni! huniarifu juu ya habari nyingi mno.—G. M. A.”
Ikiwa ungependa kupokea nakala ya karibuni ya Amkeni!, ambayo sasa huchapishwa katika lugha 81, tafadhali wasiliana na Mashahidi wa Yehova walio katika ujirani wako au andika ukitumia anwani iliyo karibu nawe iliyoonyeshwa kwenye ukurasa wa 5.