Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • g97 5/8 uku. 32
  • Amkeni! Lililisema Katika 1990

Hakuna video yoyote kwa sasa.

Samahani, haikuwezekana kupakia video.

  • Amkeni! Lililisema Katika 1990
  • Amkeni!—1997
Amkeni!—1997
g97 5/8 uku. 32

Amkeni! Lililisema Katika 1990

MAJUZI, kuenea kwa “maradhi ya kichaa cha ng’ombe” kumesababisha hofu kuu katika Ulaya. Wengi wahofu kwamba ugonjwa huo waweza kupitishwa kwa wanadamu. Baadhi ya watu waamini kwamba kuna uhusiano kati ya ulaji wa nyama za wanyama walioambukizwa na kupatwa na maradhi ya Creutzfeldt-Jakob, ambayo ni maradhi ya mfumo mkuu wa neva wa mwanadamu na ambayo huzorotesha mwili na hatimaye kuua. Haishangazi kwamba, kadiri habari za maradhi ya kichaa cha ng’ombe zilivyoenea, ulaji wa nyama ya ng’ombe ulishuka sana.

Kwa kupendeza, Stefania Ferrari aliandika katika toleo la Mei 1996 la gazeti la Kiitalia TuttoReggio: “Tumegundua gazeti fulani ambalo tayari lilikuwa likisema juu ya tauni hii yenye kuleta msiba katika 1990—Amkeni!, lichapishwalo na Mashahidi wa Yehova.” Makala aliyoirejezea ina kichwa “Tatizo la Uingereza la ‘Kichaa cha Ng’ombe’” na ilitokea katika toleo la Novemba 8, 1990, (la Kiingereza). Baada ya kunukuu mafungu manne ya kwanza, Ferrari alieleza mshangao wake kwamba makala hii ilitokea “miaka sita kabla ya jambo hili kujulikana ulimwengu pote.” Aendelea: “Kuona makala hii ya mwaka wa 1990 ambayo iliripoti kwa usahihi sana habari za karibuni, baadhi ya watu wamesema: ‘Ikiwa Mashahidi wa Yehova walijua jambo zito na la maana kama hili, kwa nini hawakujulisha kila mtu, hata wale ambao si wa kutaniko lao?’ Ebu tuwe wenye kufuatia haki: Ikiwa mmoja wa Mashahidi wa Yehova angebisha mlango wetu katika 1990 kutuonyesha Biblia na makala hiyo iliyochapishwa katika magazeti yao, ni wangapi miongoni mwetu ambao hufuata dini tofauti tungelichukulia hilo kwa uzito?”

Nyuma katika 1990, wakati makala “Tatizo la Uingereza la ‘Kichaa cha Ng’ombe’” ilipochapishwa, Amkeni! lilikuwa likichapishwa kwa wastani wa karibu nakala milioni 12, katika lugha 62. Mashahidi wa Yehova walikuwa wenye shughuli nyingi kugawanya jarida hili la wakati unaofaa katika zaidi ya mabara 200 ulimwenguni pote. Leo, Amkeni! lina wastani wa uchapishaji wa nakala 18,350,000 katika lugha 82. Jarida hili laendelea kuchapisha habari zenye kuarifu na za hivi karibuni. Ikiwa ungependa kupokea matoleo yajayo ya Amkeni!, tafadhali wasiliana na Mashahidi wa Yehova wa mahali pako au andika kwa kutumia anwani iliyoorodheshwa katika ukurasa wa 5.

    Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
    Toka
    Ingia
    • Kiswahili
    • Shiriki
    • Mapendezi
    • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
    • Masharti ya Utumiaji
    • Sera ya Faragha
    • Mpangilio wa Faragha
    • JW.ORG
    • Ingia
    Shiriki