Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Kweli Yesu Alikufa Msalabani?
    Amkeni!—2006 | Aprili
    • Maoni ya Biblia

      Je, Kweli Yesu Alikufa Msalabani?

      MSALABA ni mojawapo ya mifano ya kidini inayojulikana sana. Mamilioni wameuabudu, wakiuona kuwa kifaa kitakatifu ambacho Yesu aliuawa juu yake. Mwandikaji Mkatoliki ambaye pia ni mchunguzi wa vitu vya kale, Adolphe-Napoleon Didron, alisema hivi: “Msalaba umepewa ibada inayokaribia, au kama ile anayopewa Kristo; kipande hiki kitakatifu cha mbao kimepewa heshima inayokaribia ile ambayo Mungu Mwenyewe hupewa.”

      Watu fulani husema kwamba msalaba huwafanya wamkaribie Mungu zaidi wanaposali. Wengine huutumia kama hirizi, wakidhani kwamba utawalinda na maovu. Lakini, je, Wakristo wanapaswa kuabudu msalaba?

  • Je, Kweli Yesu Alikufa Msalabani?
    Amkeni!—2006 | Aprili
    • “Jilindeni na Sanamu”

      Suala muhimu zaidi kwa Wakristo wa kweli linapaswa kuwa kama inafaa kuabudu kifaa kilichotumiwa kumuua Yesu. Iwe aliuawa kwenye mti wa mateso, msalaba, kwa mshale, au kisu, je, inafaa kutumia kifaa hicho katika ibada?

      Tuseme mpendwa wako aliuawa kikatili na silaha iliyotumiwa ikatolewa kortini kama ushahidi. Je, ungejaribu kuchukua silaha hiyo, uipige picha, na kutokeza nakala nyingi za picha hiyo na kuwapa watu? Je, ungetengeneza mifano mbalimbali ya silaha hiyo? Je, ungetengeneza vito kutokana na silaha hiyo? Au je, ungekubali vito hivyo vitengenezwe kiwandani na kuuziwa marafiki na watu wa ukoo ili waviabudu? Huenda ikawa ungechukizwa na wazo hilo! Lakini, hivyo ndivyo watu wamefanya kuhusiana na msalaba!

      Isitoshe, kutumia msalaba katika ibada ni sawa na kutumia sanamu, jambo linaloshutumiwa katika Biblia. (Kutoka 20:2-5; Kumbukumbu la Torati 4:25, 26) Mtume Yohana alionyesha kwa usahihi mafundisho ya Ukristo wa kweli alipowaonya Wakristo wenzake hivi: “Jilindeni na sanamu.” (1 Yohana 5:21) Na Wakristo hao walifanya hivyo hata walipokabili kifo katika viwanja vya michezo vya Roma.

      Hata hivyo, Wakristo wa karne ya kwanza waliheshimu sana kifo cha kidhabihu cha Kristo. Vivyo hivyo leo, ingawa kifaa kilichotumiwa kumtesa na kumwua Yesu hakipaswi kuabudiwa, Wakristo wa kweli hukumbuka kifo cha Yesu ambacho kupitia hicho Mungu ameandaa wokovu kwa wanadamu wasio wakamilifu. (Mathayo 20:28) Wonyesho huo mkuu wa upendo wa Mungu utawaletea watu wanaopenda kweli baraka nyingi, kutia ndani tarajio la kuishi milele.—Yohana 17:3; Ufunuo 21:3, 4.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki