-
Je, Wajua?Amkeni!—2000 | Juni 8
-
-
Majibu ya Maswali
1. “Roho na kweli”
2. “Nguvu ipitayo iliyo ya kawaida”
3. Yothamu
4. Yubile
5. Ishtobu
6. Sanamu kubwa sana inayofanana na mwanadamu, ambayo sehemu zake zilifanyizwa kwa metali mbalimbali
7. Mwana-simba
8. Kondoo mume
9. Alimwacha hai mfalme wao Agagi, pamoja na mifugo na kundi la wanyama waliokuwa bora
10. Tishri
11. Katika hekalu
12. “Binti Sayuni”
13. Hazina za kimwili huharibika na haziwezi kumletea mtu kibali cha Mungu
14. Alimwondolea baraka zake na akaanza kutokeza wapinzani dhidi ya Solomoni
15. Moyo wa kitamathali
16. Aliikata na kuitupa katika moto
17. “Mnyama mkali”
18. Yeriko
-
-
Wakazi wa Mapangoni wa Siku ya KisasaAmkeni!—2000 | Juni 8
-
-
Hapa, familia kadhaa huishi kwa mtindo wa karne zilizopita. Kwa kweli, wao hujenga nyumba zao ndani ya mapango kwenye miteremko ya mlima. Vijiti na vifaa vingine, kama vile mafunjo, hufanyiza kiunzi cha ukuta mpana wa mbele. Ukuta huo hukandikwa kwa mchanganyiko wa udongo na samadi ya ng’ombe. Kuukandika hivyo huzuia baridi kali ya Lesotho, wakati halihewa hushuka chini ya kiwango cha kuganda. Ndani, kuna sehemu iliyochimbwa sakafuni iitwayo ifo, kumaanisha “mekoni,” ambayo hutumiwa vilevile kuandaa joto kunapokuwa na baridi.
Paa, ukuta wa nyuma, na kuta za pembeni hufanyizwa na jabali la pango lenyewe. Mchanganyiko wa udongo na samadi ya ng’ombe hukandikwa ukutani kila mwaka. Hilo huongeza umaridadi na kulainisha mwamba. Ngozi za ng’ombe hupamba kuta za ndani na pia hutumiwa kama magodoro ya kulalia.
Mgeni kutoka nchi za Magharibi ataburudishwa mno na maisha hayo ya kitamaduni yaliyo tofauti sana. Mtindo wa mavazi unaopendwa ni mablanketi yenye rangi mbalimbali na kofia za nyasi zenye umbo la pia. Wavulana wachungaji wanaotembea miguu mitupu mara nyingi huonwa wakichunga mifugo yao. Wanaume wa vijijini wanaweza kuonwa wakifanya kazi ama kwenye mashamba yao ya mahindi au wakizungumza kwa msisimuko na wanaume wenzao.
Dalili za tekinolojia ya kisasa huonekana pindi kwa pindi. Ndege ndogo hupaa angani pindi kwa pindi na magari yanayoendeshwa kwa magurudumu manne yanayoleta wageni mapangoni hufurahisha wadogo kwa wakubwa kijijini. Upishi mwingi hufanyiwa nje si kwa stovu bali katika vyungu vyeusi vya chuma vyenye miguu mitatu. Kwa sababu ya ukosefu wa kuni, samadi ya ng’ombe iliyokaushwa, mafunjo, na matawi machache ya miti hutumiwa kukoka moto. Vyombo vya nyumbani vya kawaida vinavyopatikana katika makao haya ya mapangoni vyatia ndani kisagio cha mahindi cha mkono na mwiko wa kukorogea uji wa mahindi.
Lesotho yajulikana sana kwa michoro ya Wenyeji wa Afrika Kusini, inayopatikana katika mapango na miamba mingi kotekote nchini. Wenyeji wa Afrika Kusini ni watu ambao kwa asili walikaa kwenye mapango ya Ha Kome. Michoro yao huonyesha utendaji mwingi mbalimbali, kama vile kuvua samaki kwa mashua na nyavu na dansi mbalimbali ambapo wachezaji walivaa vinyago vya uso wa wanyama. Michoro hiyo pia yaonyesha wanyama, kama vile nyani, simba, viboko, na pofu, aliye mkubwa zaidi katika jamii ya swala. Michoro mingi katika mapango ya Ha Kome imefutika. Ni alama fulani tu zilizobaki kama kikumbusho cha sanaa ya Wenyeji wa Afrika Kusini.
Kikundi cha Mashahidi wa Yehova hushughulika katika kazi ya kuhubiri katika eneo lisilo mbali sana na Ha Kome. Mara kwa mara, wao hutembelea wakazi wa mapangoni, ambao wanajulikana kwa ukaribishaji-wageni wao kwa watu wanaowatembelea. Mara nyingi Mashahidi hukaribishwa kwa bakuli la uji wa kienyeji unaoitwa motoho. Wengi katika Ha Kome hukubali vichapo vya Biblia. Mara nyingi wao huonyesha uthamini kwa vichapo kwa kutoa mboga, mayai, au bidhaa nyingine kuwa michango kwa kazi ya Mashahidi ya elimu.
Wakazi hao wa mapangoni wa siku ya kisasa wanastahi sana Biblia nao hupenda kuuliza maswali mengi juu ya uhai, kifo, na itikadi zao za kitamaduni. Utendaji wenye bidii wa Mashahidi katika eneo hilo umetokeza mafunzo kadhaa ya Biblia. Kwa njia hii, mbegu za kweli zimepata udongo wenye rutuba katika mioyo ya watu hao wanyenyekevu.—Mathayo 13:8.
-