-
Je, Wajua?Amkeni!—2000 | Agosti 8
-
-
Majibu ya Maswali
1. Yesu Kristo, ambaye Yohana alimtaja kuwa “mtu fulani kama mwana wa binadamu”
2. “Fuliza kushinda lililo ovu kwa lililo jema”
3. Alikuwa akionyesha uhitaji wa kunyenyekea kwa hiari madai yaliyo halali
4. “Vao lisilofisidika la roho ya utulivu na ya upole”
5. “Mwamba ule ambao mlitolewa kwa kuchongwa”
6. Kwa sababu yaliwakilisha damu yao, ambayo walikuwa wameihatarisha ili kuyapata
7. Akioga
8. “Kwa roho ya Mungu aliye hai”
9. Upepo wa magharibi wenye nguvu nyingi uliwapeleka katika Bahari ya Shamu
10. Alikosa uaminifu kumwelekea Yehova kwa kutofuata maagizo yake na kwa kumwendea mwasiliani-roho
11. Mira katika Likia
12. Aliwaandalia hali njema na riziki yao
13. Akeldama, au “Shamba la Damu”
14. Alionyesha mwelekeo mbaya kwa kujaribu kununua hiyo “zawadi ya bure ya Mungu,” na moyo wake haukuwa “mnyoofu mbele ya macho ya Mungu”
15. Alikuwa na umri wa miaka 90
16. Moabu
-
-
Mua—Mmea Mkubwa Katika Jamii ya NyasiAmkeni!—2000 | Agosti 8
-
-
2,100, ambao kwa sehemu kubwa unapakana na lile Tumbawe Kuu lililo mashuhuri. (Ona makala “A Visit to the Great Barrier Reef,” katika toleo la Amkeni! la Juni 8, 1991, Kiingereza.) Eneo hilo huwa na tabia-nchi ya hewa yenye mvuke wenye joto mwaka mzima, hali ambayo inafanya miwa isitawi, na wakulima wapatao 6,500 humiliki mashamba madogo ya familia ambayo yamesambaa katika pwani kama vichala vya zabibu kwenye mzabibu.
Baada ya kusafiri kwa muda mrefu, twaona kwa mbali jiji lililo mashuhuri kwa uzalishaji wa sukari la Bundaberg, katika pwani ya kati ya Queensland. Tuteremkapo kilima twaona mandhari yenye kuvutia sana—miwa mingi kupindukia ikitikiswa na upepo! Twaona rangi nyingi kama nini! Mashamba mbalimbali ya miwa yamefikia hatua mbalimbali za ukomavu, kwa hiyo yanafanyiza mandhari inayoshabihi viraka vya rangi mbalimbali za kijani kibichi na dhahabu vilivyopangwa taratibu, huku maeneo yasiyolimwa mwaka huu au yaliyofyekwa karibuni yakiwa na rangi ya kahawia.
Julai ni mwezi wenye baridi kuliko yote, na msimu wa kuvuna na kusindika umeanza punde. Utaendelea hadi Desemba kadiri miwa inavyokomaa. Sasa tuna hamu ya kuzuru kiwanda cha sukari ili tuone kinachotukia kwa miwa iliyovunwa. Lakini inapendekezwa kwamba kabla ya kwenda huko tujifunze mambo fulani kuhusu miwa. Kwa hiyo twaamua kuanza kwenye kituo cha utafiti wa sukari kilichojengwa katika eneo hilo. Wanasayansi hutumia kituo hicho kukuza aina mpya ya miwa na kufanya utafiti wa kuboresha kilimo na ukuzaji wa miwa.
Chanzo Chake na Ukuzaji
Katika kituo cha utafiti wa sukari, mtaalamu mmoja wa kilimo mwenye shauku afurahi kutufundisha habari fulani kuhusu miwa na namna inavyokuzwa. Mua ambao ulianza katika misitu ya mvua ya Kusini-mashariki ya Asia na New Guinea ni mmea mkubwa katika jamii ya nyasi, inayotia ndani nyasi mbalimbali kama vile nyasi laini ya bustani, nafaka, na vichaka vya mianzi. Mimea hiyo yote hutengeneza sukari katika majani yake kwa utaratibu unaoitwa usanidi-nuru. Lakini miwa ni tofauti sana kwa sababu hutengeneza sukari nyingi sana kisha huhifadhi maji hayo matamu ya sukari katika vikonyo vyake vyenye nyuzinyuzi.
Ukuzaji wa miwa ulienea sana katika India ya kale. Waandishi katika jeshi la Aleksanda Mkuu lililoshambulia India mwaka wa 327 K.W.K., waliona wakazi wa huko “wakitafuna tete za ajabu, zilizotokeza aina fulani ya asali bila kusaidiwa na nyuki.” Ukuzaji wa miwa ulienea kasi katika karne ya 15, wakati uvumbuzi na ufanisi wa ulimwengu ulipopamba moto. Leo kuna maelfu ya jamii za miwa, na zaidi ya nchi 80 huchangia takriban tani bilioni moja za miwa zinazovunwa kila mwaka.
Katika nchi nyingi ulimwenguni, upandaji wa
-