Je, Wajua?
1. Ni jina gani la cheo walilopewa watawala wa majiji matano ya Wafilisti walioshirikiana kwa manufaa yao wenyewe, kama vile kumshinda Samsoni? (Waamuzi 16:5)
2. Walipokumbuka walichokula Misri, Waisraeli walitamani vyakula gani wakiwa nyikani? (Hesabu 11:5)
3. Yesu aliwakumbusha wanafunzi wake mambo gani ambayo mayungiyungi ya shambani hayahitaji kufanya, ijapokuwa yamepambwa vizuri? (Luka 12:27)
4. Ingawa wajane na wanawake waliotalikiwa walifungwa na nadhiri zao chini ya Sheria ya Kimusa, ni jambo gani ambalo mume angeweza kufanya kwa nadhiri yoyote iliyowekwa na mke wake? (Hesabu 30:13)
5. Katika nyakati za Biblia, ni ishara ipi iliyotumiwa kuonyeshana shauku au staha? (1 Samweli 20:41, 42)
6. Amri ya pili ilikataza nini? (Kutoka 20:4, 5)
7. Waisraeli walipokea Amri Kumi jinsi gani kwa mara ya kwanza, na chini ya hali gani? (Kumbukumbu la Torati 10:4)
8. Ni nani aliyenunua sakafu ya kupuria ya Ornani, na ni nini ambacho kilijengwa kwenye sehemu hiyo baadaye? (1 Mambo ya Nyakati 21:24; 2 Mambo ya Nyakati 3:1)
9. Solomoni alikuwa na maakida wangapi, na kazi yao ilikuwa gani? (1 Wafalme 4:7)
10. Kwa nini Petro anatushauri ‘tujifunge hali ya akili ya kujishusha chini kuelekea mtu na mwenzake’? (1 Petro 5:5)
11. Ni nani waliobishana na Paulo kwenye mahali pa soko pa Athene, wakikana tumaini la ufufuo? (Matendo 17:18)
12. Ni vitu gani alivyokabidhiwa kuhani wa cheo cha juu, ambavyo vilitumiwa kuamua mapenzi ya Yehova kuhusu jambo fulani? (Kutoka 28:30)
13. Ni nabii yupi aliyepata ono la gari la kimbingu la Yehova?
14. Ni jina gani walilopewa Hamani na baba yake, Hamedatha, lionyeshalo kwamba walikuwa wa nasaba ya Waamaleki na maadui wa jadi wa Wayahudi? (Esta 3:1; 8:3)
15. Ni kipimo gani cha maji cha hapo kale kilicholingana na lita 3.67 au takriban galoni moja (ya Marekani)? (Kutoka 29:40)
16. Chini ya Sheria ya Kimusa, mnyama alipaswa kuwaje ili aonwe kuwa safi, wa kuliwa? (Mambo ya Walawi 11:3)
17. Solomoni alitengeneza kiti chake cha ufalme akitumia nini? (1 Wafalme 10:18)
18. Yesu alianzishaje mazungumzo na mwanamke Msamaria kwenye kisima? (Yohana 4:7)
19. Kaini alimwulia Abeli wapi? (Mwanzo 4:8)
20. Ni ndege yupi wa kwanza kutajwa kwa jina kihususa katika Biblia? (Mwanzo 8:7)
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
Majibu ya Maswali
1. Wakuu
2. Samaki, matango, matikiti, mboga, vitunguu, na vitunguu saumu
3. Kumenyeka au kusokota
4. Angeweza kuitangua
5. Wangebusiana
6. Kutengeneza sanamu za kuchonga na kuziabudu
7. Zilitolewa kwenye Mlima Sinai, Yehova aliposema “toka kati ya moto”
8. Mfalme Daudi; hekalu
9. Kumi na wawili; kila mmoja alileta chakula cha nyumba ya Solomoni na vitu vinginevyo mwezi mmoja katika mwaka kwa kubadilishana
10. “Kwa sababu Mungu hupinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu fadhili isiyostahiliwa”
11. “Wanafalsafa Waepikurea na Wastoa”
12. Urimu na Thumimu
13. Ezekieli (Ezekieli, sura ya 1)
14. Mwagagi
15. Ni hin
16. Alipaswa kucheua na awe na kwato, au miguu ya kupasuka
17. Pembe na kukifunikiza kwa dhahabu
18. Alimwomba maji
19. Uwandani
20. Kunguru