Je, Wajua?
(Majibu ya maswali haya yaweza kupatikana katika maandiko ya Biblia ambayo yameonyeshwa, na orodha kamili ya majibu imechapwa kwenye ukurasa wa 27. Kwa habari zaidi, ona kichapo “Insight on the Scriptures,” kilichochapishwa na Watchtower Bible and Tract Society of New York, Inc.)
1. Maandiko husema ni nini ambacho ‘kimewekwa akiba milele’ kwa ajili ya watu wasiomwogopa Mungu na waasi-imani? (Yuda 13)
2. Ni nini ambacho hakikuwa kimetukia bado kabla ya mimea kuchipuka siku ya tatu ya uumbaji? (Mwanzo 2:5)
3. Kwa nini Yehova aliwatumia Waisraeli nyoka wenye sumu? (Hesabu 21:5-7)
4. Yehova peke yake anasemwa yukoje katika maana kamili? (Zaburi 18:30)
5. Paulo anasema upendo haushangilii nini? (1 Wakorintho 13:6)
6. Ni watu gani watatu waliomletea Daudi vitu vilivyohitajiwa sana alipolazimika kukimbia Yerusalemu kwa sababu ya uasi wa Absalomu? (2 Samweli 17:27-29)
7. Yehova anaitwaje kwa sababu ya kuwa ngome na kimbilio la watu wake? (Zaburi 62:7)
8. Kwa nini Efraimu alimwita mwanaye aliyezaliwa karibuni Beria, jina limaanishalo “Kwa Maafa”? (1 Mambo ya Nyakati 7:20-23, Biblia Habari Njema)
9. Yesu alitoa kielezi gani ili kuonyesha kwamba Mungu atahakikisha kwamba anawavisha watumishi wake? (Luka 12:27, 28)
10. Jeshi la kivita lililoongozwa na Zera Mkushi lililoshindwa na Yehova mbele ya Asa lilikuwa kubwa kadiri gani? (2 Mambo ya Nyakati 14:9, 12)
11. Mtume Paulo alitoa onyo gani kuhusu mashirika ya mtu? (1 Wakorintho 15:33)
12. Ufalme wa Mungu utazifanyia nini falme zote za wanadamu? (Danieli 2:44)
13. Nyumba ya Rahabu ilitambulishwaje ili yeye na watu wa jamaa yake wapate kuokolewa wakati jiji la Yeriko lilipoharibiwa? (Yoshua 2:18)
14. Yoshua aliutekaje mji wa Ai? (Yoshua 8:3-7)
15. Yehova alimwamuru Musa ahifadhi kiasi gani cha mana kwa ajili ya vizazi vijavyo? (Kutoka 16:32-34)
Majibu ya Maswali
1. “Weusi wa giza”
2. Mvua haikuwa imenyesha
3. Kwa sababu waliasi na kumnung’unikia Yehova
4. Mkamilifu
5. Ukosefu wa uadilifu
6. Shobi, Makiri, na Barzilai
7. Mwamba
8. Kwa sababu watu wa Gathi walikuwa wamewaua nduguze wakubwa
9. Alisema juu ya mapambo ya yungiyungi
10. Wanaume milioni moja
11. “Mashirika mabaya huharibu mazoea yenye mafaa”
12. Utazivunja vipande vi- pande na kuziharibu
13. Alifunga kamba nyekundu katika dirisha
14. Aliweka wanaume waotee upande wa nyuma wa mji kisha akawavuta wakazi wa mji huo kwa kujisingizia kuwa anawakimbia hadi walipoenda mbali na mji wao
15. Kipimo cha pishi moja