-
Je, Wajua?Amkeni!—2004 | Agosti 8
-
-
Majibu ya Maswali
1. Eli
2. Seniri
3. Ketura; sita
4. Kwa sababu divai inapochachuka, itapasua ngozi isiyonyumbulika ya viriba hivyo
5. Egloni alikuwa mnene sana hivi kwamba upanga wote uliingia tumboni
6. Kwa kuwa “hakuna wokovu katika mwingine yeyote.” Fidia ilitolewa kupitia Yesu na yeye ndiye Hakimu aliyewekwa rasmi
7. Ni Yehova tu asiye na mipaka, ukuu wake hauwezi kulinganishwa na yeyote, anastahili sifa zote, naye ni mkuu katika sifa na nguvu zake
8. Kwa kuwa mafuta yalionwa kuwa sehemu yenye thamani zaidi ya mnyama, hilo lilionyesha kwamba sehemu iliyo bora zaidi ni ya Yehova
9. Tai
10. Mungu
11. Ahiya
12. Kuku
13. Jicho
14. “Wakati wa mwisho”
15. Wakati wa usiku wanafunzi wake walimshusha katika kapu kupitia shimo ukutani
16. “Kupenda pesa”
17. Kumi na wawili; Yoshua na Kalebu
18. Nero
-
-
Mabadiliko MakubwaAmkeni!—2004 | Agosti 8
-
-
kila meta moja ya mraba ya liginaiti inayochimbuliwa katika eneo la Rhineland nchini Ujerumani, zaidi ya meta 6 za mraba za matabaka hukwanguliwa. Ukanda-safirishi huzunguka kwa mwendo wa kasi sana kuliko hata mwendo wa baiskeli. Kanda-safirishi hizo hukutana mahali pa kukusanya liginaiti na matabaka hayo ya juu. Kisha kwa kutumia magari-moshi, liginaiti hupelekwa kwenye ghala la makaa au vituo vya umeme nayo matabaka hupelekwa kwenye eneo la takataka. Liginaiti nyingi hupelekwa kwenye vituo vya umeme ili kuzalisha umeme.
Matabaka hayo ya juu hutumiwa kujaza mahali ambapo liginaiti imechimbuliwa. Mashine humwaga udongo hatua kwa hatua hadi shimo linapojaa. Udongo unaosalia hupelekwa kwenye maeneo ya takataka. Takataka hizo zinaweza kurundamana kufikia urefu wa meta 200. Watunzaji wa bustani huwa na kazi ngumu ya kutandaza marundo hayo katika maeneo ya mashambani na kuyafanya yafae kilimo na upandaji wa miti.
Kushusha Tabaka la Maji
Uchimbaji wa migodi huathiri sana mandhari na mifumo ya kiasili. Ili kuudumisha mgodi bila maji, tabaka la maji hushushwa hadi sehemu ya chini sana ya mgodi. Kiasi cha maji kinachoondolewa nchini Ujerumani kila mwaka, kinaweza kuwatosheleza wakaaji wa Berlin, jiji kuu la Ujerumani, kwa miaka mitatu na nusu hivi. Kuondolewa kwa maji mengi hivyo kunawahangaisha wanamazingira ambao wanahofia jinsi Mbuga ya Maas-Schwalm-Nette iliyo kwenye mpaka wa Ujerumani na Uholanzi inavyoathiriwa. Hilo ni eneo lenye umajimaji ambalo lina mimea mingi na ndege.
Wasimamizi wa migodi wamesema kwamba hakuna sababu ya kuhangaika. Kwa kuwa maji yaliondolewa wakati wa kuchimba migodi, maji mengine hurudishwa ardhini mwendo mfupi kutoka kwenye mgodi. Maji hayo hurudishwa kupitia visima. Kwa kufanya hivyo inatumainiwa kuwa eneo hilo halitakauka.
Mandhari Mpya Yasitawi
Dunia inabadilika daima. Tani milioni 25,000 za takataka husukumwa baharini kila mwaka bila sisi kujua. Hata hivyo, mabadiliko ya mandhari huonekana waziwazi kwa mtu anayesimama kando ya mgodi. Mandhari mpya husitawi. Hilo limeathirije eneo la migodi ya liginaiti huko Rhineland?
Maeneo ya migodi yaliyokuwa yamechimbuliwa katika bonde lililoko kati ya Cologne na Aachen yamebadilishwa na kutumiwa kwa ajili ya kilimo, misitu, na mbuga. Isitoshe, mikondo ya maji, barabara, na reli imegeuzwa na kuelekezwa kwingine. Kitabu Lignite Mining in the Rhineland kinasema: “[Marekebisho] hayo hayakusudiwi kuigiza asili. Mwanadamu anaweza kutimiza sehemu ndogo tu. Sehemu kubwa hutukia kiasili.” Kufikia sasa, zaidi ya asilimia 65 ya ardhi iliyoathiriwa imeanza kutumiwa hasa kwa kilimo. Ili kutimiza kusudi hilo, udongo wenye rutuba ulitandazwa vizuri kufikia meta mbili juu ya udongo unaoweza kupenyeza maji. Kwa miaka mingi maeneo hayo yalilimwa na makampuni yenye mashamba ambayo baadaye yaliyaacha ili yatumiwe kwa ajili ya kilimo cha kawaida.
Sehemu ndogo ya misitu iliyositawi karibuni
-