-
Je, Wajua?Amkeni!—2003 | Februari 8
-
-
Majibu kwa Maswali
1. Kwenye maji ya Meriba
2. Waseba
3. Mishaeli
4. Shangwe
5. Baharini
6. “Talanta ya fedha, na mavazi mawili”
7. Sihoni
8. Efroni Mhiti
9. Huleta mtego. Kumtumaini Yehova
10. Amani
11. Alimwua Zimri mkuu wa kabila la Simeoni na mwanamke Mmidiani ambaye Zimri alimleta kwenye hema lake ili afanye uasherati naye
12. Vipimo
13. “Kuendelea kujiepusha na vitu vilivyotolewa dhabihu kwa sanamu na damu na kutokana na vitu vilivyonyongwa na uasherati”
14. ‘Kuona hekima yote ya Sulemani’
15. Hawakupaswa kufanya kazi yoyote ngumu
16. Marko
17. Malko, mtumwa wa kuhani wa cheo cha juu
18. Kiebrania, Kiaramu, na Kigiriki
19. Waarabu
20. Ili waache kiasi fulani cha nafaka “kwa ajili ya maskini na mgeni”
-
-
Je, Kuna Dhambi Isiyosameheka?Amkeni!—2003 | Februari 8
-
-
Yaelekea Paulo alizungumzia dhambi ya aina hiyo alipoandika maneno haya: “Haiwezekani kwa habari ya wale ambao wametiwa nuru mara moja kwa wakati wote, na ambao wameonja zawadi ya bure ya kimbingu, na ambao wamekuwa washiriki wa roho takatifu, na ambao wameonja neno bora la Mungu na nguvu za mfumo wa mambo unaokuja, lakini ambao wameanguka, kuwarudisha tena kwenye toba.” (Waebrania 6:4-6) Mtume huyo alisema hivi pia: “Tukizoea dhambi kwa kusudi baada ya kuwa tumepokea ujuzi sahihi juu ya kweli, hakuna tena dhabihu yoyote iliyoachwa kwa ajili ya dhambi.”—Waebrania 10:26.
Mwenendo wa baadhi ya viongozi wa dini wa siku zake ndio uliomfanya Yesu atoe onyo juu ya dhambi isiyosameheka. Lakini hawakutii onyo lake. Badala yake walimwua. Baadaye walipata habari isiyokanushika kwamba roho takatifu ilikuwa imefanya mwujiza. Waliambiwa kwamba Yesu alikuwa amefufuliwa! Ilikuwa wazi kwamba Yesu alikuwa Kristo! Hata hivyo, waliipinga roho takatifu kwa kuwalipa askari Waroma waseme uwongo kuhusu ufufuo wa Yesu.—Mathayo 28:11-15.
Onyo kwa Wakristo wa Kweli
Kwa nini Wakristo wa kweli hutia maanani onyo hilo kuhusu dhambi isiyosameheka? Kwa sababu ijapokuwa tuna ujuzi sahihi juu ya Mungu na utendaji wa roho yake, bado moyo wetu unaweza kubadilika kuwa mwovu hatua kwa hatua. (Waebrania 3:12) Hatupaswi kamwe kufikiri kwamba jambo hilo haliwezi kutupata sisi. Fikiria Yudasi Iskariote. Awali alikuwa mfuasi mwaminifu wa Yesu. Alichaguliwa kuwa mmoja wa wale mitume 12, kwa hiyo, bila shaka alikuwa na sifa nzuri. Lakini wakati fulani alianza kuruhusu mawazo maovu na tamaa zikue, na mwishowe zikamshinda. Katika pindi ambazo alishuhudia miujiza ya ajabu ya Yesu, alikuwa akiiba pesa. Kisha, akamsaliti Mwana wa Mungu kimakusudi ili apate pesa.
Baadhi ya watu waliokuwa Wakristo waaminifu awali wamejitenga na Mungu kimakusudi. Huenda walifanya hivyo kwa sababu ya kuudhika, au kwa sababu ya kiburi au pupa. Sasa wao ni waasi-imani wanaoipinga roho ya Mungu. Wao hupinga kimakusudi kile ambacho wanajua vizuri ni kazi ya roho takatifu. Je, watu hao wamefanya dhambi isiyosameheka? Yehova ndiye Hakimu.—Waroma 14:12.
Badala ya kuwahukumu wengine, ni heri kila mmoja wetu ajiepushe na dhambi za siri ambazo zinaweza kufanya mioyo yetu kuwa migumu hatua kwa hatua. (Waefeso 4:30) Na tunafarijiwa kujua kwamba Yehova atasamehe kabisa hata makosa mazito ambayo tumetenda, iwapo tutatubu.—Isaya 1:18, 19.
-