Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Je, Wajua?
    Amkeni!—2003 | Agosti 8
    • Majibu ya Maswali

      1. Uajemi

      2. Mtambo mdogo wa usukani wa meli kubwa

      3. Hawa

      4. Katika “hati-kunjo ya uhai”

      5. Mamba

      6. Alikataa kufika mbele ya mfalme

      7. Yoshua na Kalebu

      8. Miaka 1,000

      9. Vazi lake

      10. Kati ya zile fimbo zote za wale viongozi wa makabila 12, fimbo ya Haruni tu ndiyo iliyochanua maua na kuzaa lozi mbivu

      11. Binti yake mkubwa, Merabu

      12. La upole

      13. Mungu

      14. Galio, prokonso wa Akaya

      15. Mina

      16. Buli, mwezi wa nane wa kalenda takatifu

  • Je, Inafaa Kuwachukia Watu wa Jamii Nyingine?
    Amkeni!—2003 | Agosti 8
    • yenye huruma kwa Waisraeli: “Na mgeni akikaa pamoja nawe katika nchi yako, usimdhulumu. Mgeni akaaye pamoja nawe atakuwa kama mzalia kwenu; mpende kama nafsi yako; kwa maana ninyi mlikuwa wageni katika nchi ya Misri; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.” Amri kama hizo zinapatikana pia katika kitabu cha Kutoka na Kumbukumbu la Torati. Ni wazi kwamba Yehova hakuunga mkono chuki ya kijamii. Alitaka watu wa jamii zote waishi kwa amani.

      Yesu Aliwahimiza Watu wa Jamii Zote Wapendane

      Wakati Yesu alipokuwa duniani, kulikuwa na chuki fulani kati ya Wayahudi na Wasamaria. Katika pindi moja, Wasamaria walimfukuza Yesu kutoka katika kijiji chao kwa sababu tu alikuwa Myahudi aliyekuwa akielekea Yerusalemu. Ungehisije kama ungetendewa hivyo? Huenda wanafunzi wa Yesu walichochewa na chuki hiyo kati ya Wasamaria na Wayahudi walipomuuliza hivi: “Bwana, je, wataka tuambie moto uteremke kutoka mbinguni na kuwaangamiza?” (Luka 9:51-56) Je, Yesu aliruhusu maoni yao mabaya yamwathiri? Hata kidogo, badala yake aliwakemea na kwenda kwenye kijiji kingine kwa amani. Muda mfupi baadaye, Yesu alitoa kielezi cha Msamaria mwema. Kielezi hicho kilionyesha kwa mkazo sana kwamba jamii ya mtu haimfanyi kuwa adui. Ama kweli, aweza kuwa jirani mwema sana!

      Jamii Mbalimbali Katika Kutaniko la Kikristo

      Wakati wa huduma yake duniani, Yesu alifanya wanafunzi hasa kutoka kwa watu wa taifa lake. Lakini baadaye alisema kwamba wengine pia wangekuwa wanafunzi wake. (Mathayo 28:19) Je, watu wa jamii zote wangekubaliwa? Ndiyo! Mtume Petro alisema hivi: “Kwa hakika nahisi kwamba Mungu si mwenye ubaguzi, bali katika kila taifa mtu ambaye humhofu na kutenda uadilifu akubalika kwake.” (Matendo 10:34, 35) Baadaye mtume Paulo alikazia jambo hilo kwa kusema waziwazi kwamba katika kutaniko la Kikristo watu wote ni sawa hata wawe wa jamii gani.—Wakolosai 3:11.

      Jambo jingine linaloonyesha kwamba Mungu huwakubali watu kutoka kwa jamii zote lapatikana kwenye kitabu cha Biblia cha Ufunuo. Katika njozi iliyoongozwa na Mungu, mtume Yohana aliona “umati mkubwa . . . kutoka katika mataifa yote na makabila na vikundi vya watu na lugha” uliokolewa na Mungu. (Ufunuo 7:9, 10) ‘Umati huo mkubwa’ utakuwa msingi wa jamii mpya ya wanadamu itakayokuwa na watu wa jamii zote ambao wataishi kwa amani, wakiunganishwa na upendo wao kwa Mungu.

      Kwa sasa, Wakristo hawapaswi kuwahukumu wengine kwa sababu wao ni wa jamii fulani. Badala ya kumwona mtu kuwa wa jamii fulani, ni jambo la haki na la upendo kuzingatia sifa zake kama Mungu anavyofanya. Bila shaka wewe pia unataka kuonwa hivyo. Yesu alihimiza hivi: “Kwa hiyo, mambo yote mtakayo watu wawafanyie nyinyi, lazima mwafanyie wao pia hivyohivyo.” (Mathayo 7:12) Kuishi bila chuki ya kijamii ni jambo lenye kufurahisha. Hilo huleta amani nyingi ya akili na amani pamoja na wengine. La muhimu hata zaidi, hiyo hutufanya tuwe kama Muumba wetu Yehova Mungu asiye na ubaguzi. Hiyo ni sababu kuu inayopaswa kutufanya tukatae katakata kuwachukia watu wa jamii nyingine!

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki