-
Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
“Na mimi nikaona, na, tazama! farasi mweupe; na mmoja aliyeketi juu yake alikuwa na upinde; na taji lilipewa kwa yeye, na yeye akatoka kwenda akishinda na kukamilisha ushindi wake.” (Ufunuo 6:2, NW)
-
-
Wana-Farasi Wanne Katika Mwendo!Ufunuo—Upeo Wao Mtukufu U Karibu!
-
-
4. Ni nani aliye Mpandaji-farasi mweupe? Eleza.
4 Ni nani aliye Mpandaji-farasi huyu? Yeye ana upinde, silaha ya vita ya kushambulia, lakini anapewa pia taji. Wale waadilifu pekee wanaoonekana wakivaa taji katika pindi ya ile siku ya Bwana ni Yesu na ile jamii inayowakilishwa na wale wazee 24. (Danieli 7:13, 14, 27; Luka 1:31-33; Ufunuo 4:4, 10; 14:14)a Haielekei kwamba mshiriki wa kile kikundi cha wazee 24 angeonyeshwa kuwa akipokea taji kwa ustahili wake mwenyewe. Kwa sababu hiyo, huyu mpanda-farasi aliye pekee lazima awe Yesu Kristo na si mwingine. Yohana anamwona katika mbingu wakati ule wa kihistoria wenye maana kubwa katika 1914 wakati Yehova anapotangaza “Mimi, hata mimi, nimeweka mfalme wangu,” na kumwambia kwamba hili ni kwa kusudi la “kwamba mimi nipate kukupa mataifa yawe urithi wako.” (Zaburi 2:6-8, NW)b Hivyo, katika kufungua kile kifungo cha kwanza Yesu anafunua jinsi yeye mwenyewe, akiwa Mfalme ambaye amevikwa taji sasa hivi, anatoka kwenda kupiga vita katika wakati wa Mungu uliowekwa.
-