Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Arusi Zenye Kuheshimika Machoni pa Mungu na Wanadamu
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Oktoba 15
    • Ndoa ya Kimila na ya Kiserikali

      12. Ndoa ya kimila ni ndoa ya aina gani, na wale walio katika ndoa hiyo wanapaswa kufanya nini?

      12 Katika nchi fulani, huenda wale wanaotaka kufunga ndoa wakaamua kufanya ndoa ya kimila. Hilo halirejelei watu wawili wanaoishi tu pamoja, wala halirejelei wale wanaoishi pamoja kama mume na mke kwa njia isiyo halali. Huenda zoea hilo likakubaliwa katika maeneo mengine ingawa si ndoa halali kabisa.d Tunazungumzia ndoa ambayo inafuata desturi zinazotambuliwa na wengi katika kabila au eneo fulani. Huenda hilo likatia ndani kulipa kabisa na kukubaliwa kwa mahari, na hivyo wenzi hao wanakuwa wamefunga ndoa halali kisheria na Kimaandiko. Serikali huona ndoa hiyo ya kimila kuwa halali kisheria na isiyoweza kuvunjwa. Kwa kawaida, ndoa hiyo ya kimila inaweza baadaye kuandikishwa na wenzi kupewa cheti rasmi. Kuandikisha ndoa kunaweza kuwa ulinzi kwa wenzi hao au kwa mke ikiwa atakuwa mjane na kwa watoto wowote ambao huenda wakazaliwa baadaye. Kutaniko linapaswa kumhimiza yeyote ambaye amefanya ndoa ya kimila aiandikishe haraka iwezekanavyo. Inaonekana kwamba chini ya Sheria ya Musa, ndoa na kuzaliwa kwa watoto kuliandikishwa kirasmi.—Mathayo 1:1-16.

      13. Baada ya kufunga ndoa ya kimila, hotuba ya arusi inafaa ishughulikiweje?

      13 Wenzi waliounganishwa kwa njia halali katika ndoa ya kimila wanakuwa mume na mke wanapofunga ndoa hiyo.

  • Arusi Zenye Kuheshimika Machoni pa Mungu na Wanadamu
    Mnara wa Mlinzi—2006 | Oktoba 15
    • 14. Mkristo anaweza kufanya nini ikiwa ndoa za kimila na kiserikali zinakubalika?

      14 Katika nchi fulani ambako ndoa za kimila zinaonwa kuwa ndoa halali, kuna pia ndoa za kiserikali (au kisheria). Kwa kawaida, ndoa za kiserikali hufungwa mbele ya ofisa wa serikali, na huenda zikahusisha kuweka nadhiri ya ndoa na kutia sahihi cheti. Wakristo fulani wanapendelea ndoa za kiserikali badala ya ndoa za kimila. Si takwa la kisheria kufuata taratibu zote mbili; kila moja ya ndoa hizo ni halali kisheria.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki