Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • Maoni ya Mkristo Kuhusu Desturi za Mazishi
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Julai 15
    • Je, Mavazi ya Kuomboleza Yanakubalika?

      Mashahidi wa Yehova huombolezea kifo cha wapendwa wao. Kama Yesu, huenda wakalia. (Yohana 11:35, 36) Lakini hawalioni kuwa jambo la lazima kuonyesha huzuni yao hadharani kwa ishara fulani ya nje. (Linganisha Mathayo 6:16-18.) Katika nchi nyingi, wajane hutarajiwa kuvaa mavazi maalumu ili kuwatuliza wafu. Mavazi hayo lazima yavaliwe kwa miezi kadhaa au hata mwaka baada ya mazishi, na karamu hufanywa wakati wa kuyavua.

      Kutoonyesha ishara za kuomboleza huonekana kuwa kosa dhidi ya yule aliyekufa. Kwa sababu hiyo, katika sehemu za Swaziland, machifu wa makabila wamewafukuza Mashahidi wa Yehova kutoka katika nyumba na ardhi zao wenyewe. Hata hivyo, Wakristo hao waaminifu sikuzote wametunzwa na ndugu zao wa kiroho wanaoishi sehemu nyinginezo.

      Mahakama Kuu ya Swaziland iliamua kwa kupendelea Mashahidi wa Yehova, ikisema kwamba wapaswa kuruhusiwa kurudi kwenye nyumba na ardhi zao. Katika kisa kingine, mjane Mkristo aliruhusiwa kubaki kwenye ardhi yake baada tu ya kuonyesha barua na utepe uliorekodiwa ambamo mume wake aliyekufa alikuwa ameeleza waziwazi kwamba mke wake hapaswi kuvaa mavazi ya kuomboleza. Hivyo, aliweza kuthibitisha kwamba kwa kweli alikuwa akimstahi mume wake.

  • Maoni ya Mkristo Kuhusu Desturi za Mazishi
    Mnara wa Mlinzi—1998 | Julai 15
    • Walibarikiwa kwa Sababu ya Msimamo Wao Imara

      Sibongili Ni mjane Mkristo jasiri anayeishi Swaziland. Baada ya kifo cha mume wake cha hivi majuzi, alikataa kufuata desturi zifikiriwazo na wengi kuwa zinawatuliza wafu. Kwa mfano, hakunyoa nywele zake. (Kumbukumbu la Torati 14:1) Washiriki wanane wa familia walikasirishwa na jambo hilo na kumnyoa kwa nguvu. Pia waliwazuia Mashahidi wa Yehova wasimtembelee Sibongili nyumbani ili kumfariji. Hata hivyo, watu wengine wenye kupendezwa na ujumbe wa Ufalme walifurahia kumtembelea na kumpelekea barua za kufariji zilizoandikwa na wazee. Siku ambayo Sibongili alitarajiwa kuvaa mavazi maalumu ya kuomboleza, jambo lenye kushangaza lilitukia. Mshiriki mashuhuri wa familia alifanya mkutano kuzungumzia kukataa kwake kukubaliana na desturi za kimapokeo za kuomboleza.

      Sibongili aliripoti hivi: “Waliniuliza kama imani yangu ya kidini iliniruhusu kuonyesha huzuni yangu kwa kuvaa mavazi meusi ya kuomboleza. Baada ya kueleza msimamo wangu, waliniambia hawatanilazimisha. Nilishangaa kwamba, wote waliniomba msamaha kwa kunitenda vibaya na kwa kuninyoa kwa lazima. Wote waliniomba msamaha.” Baadaye, dada yake Sibongili alisema aliamini kwamba dini ya Mashahidi wa Yehova ndiyo ya kweli, naye akaomba funzo la Biblia.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki