-
‘Walisafiri kwa Mashua Kwenda Kipro’Mnara wa Mlinzi—2004 | Julai 1
-
-
Leo, jiji la Salami limebaki magofu tu. Hata hivyo, uvumbuzi wa akiolojia unaonyesha kwamba jiji hilo lilikuwa maarufu na lenye ufanisi. Yaonekana eneo la soko, ambalo lilikuwa kituo cha siasa na utendaji wa kidini, ndilo lililokuwa soko kubwa zaidi la Kiroma la mikutano kuwahi kuchimbuliwa katika eneo la Mediterania. Magofu yake ambayo ni ya tangu wakati wa Augustus Caesar, yameonyesha mchanganyiko wenye kutatanisha wa sakafu, kumbi za kufanyia mazoezi, madimbwi makubwa yenye kuvutia, uwanja wa michezo, ukumbi wa maonyesho, makaburi yenye fahari, na jumba kubwa la maonyesho linaloweza kutoshea watu 15,000! Karibu na magofu hayo kuna hekalu lenye fahari la Zeu.
-
-
‘Walisafiri kwa Mashua Kwenda Kipro’Mnara wa Mlinzi—2004 | Julai 1
-
-
Jiji la Kourion lilikuwa upande wa juu zaidi wa bahari, kwenye miteremko inayoshuka moja kwa moja kwenye fuo. Jiji hilo lenye fahari la Wagiriki na Waroma liliharibiwa na tetemeko la nchi lilelile lililoharibu Salami mnamo mwaka wa 77 W.K. Kuna magofu ya hekalu lililojengewa Apolo kuanzia mwaka wa 100 W.K. Uwanja wa michezo ungeweza kutoshea watazamaji 6,000. Nakshi maridadi za mawe zilizorembesha sakafu za nyumba za kifahari za watu binafsi zinaonyesha kwamba watu wengi huko Kourion waliishi maisha ya starehe.
-
-
‘Walisafiri kwa Mashua Kwenda Kipro’Mnara wa Mlinzi—2004 | Julai 1
-
-
Uchimbuzi mbalimbali wa mji wa Pafosi umeonyesha maisha ya starehe ya matajiri wa karne ya kwanza—barabara kubwa za jiji, nyumba za kifahari za watu binafsi zilizopambwa vizuri, shule za muziki, kumbi za kufanyia mazoezi, na ukumbi wa maonyesho.
-