Watchtower MAKTABA KWENYE MTANDAO
Watchtower
MAKTABA KWENYE MTANDAO
Kiswahili
  • BIBLIA
  • MACHAPISHO
  • MIKUTANO
  • “Meli za Kitimu” Zatawala Baharini
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Oktoba 15
    • Mnamo 1982 meli iliyovunjika mwishoni mwa karne ya 14 K.W.K. ilipatikana karibu na pwani ya kusini ya Uturuki. Vitu vingi vyenye thamani vilipatikana chini ya maji. Vitu hivyo vinatia ndani vipande vya shaba nyekundu vinavyoaminika kuwa vilitoka Saiprasi, kaharabu, magudulia ya Wakanaani, mbao za mpingo, pembe za tembo, vito vingi vya Wakanaani vya dhahabu na fedha, na mapambo fulani mfano wa mbawakavu ambaye Wamisri walimwona kuwa mtakatifu, na pia vitu vingine kutoka Misri. Baada ya kuchunguza udongo uliopatikana katika meli hiyo, wachunguzi fulani wamesema kwamba inaelekea meli hiyo ilitoka Saiprasi.

  • “Meli za Kitimu” Zatawala Baharini
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Oktoba 15
    • Meli za Biashara

      Maumbo mengi ya udongo ya meli na mashua yamepatikana katika maeneo ya makaburi ya jiji la kale la Amathus huko Saiprasi. Maumbo hayo yanasaidia sana kufahamu aina mbalimbali za meli za Wasaiprasi. Baadhi ya maumbo hayo ya meli yamewekwa katika majumba ya ukumbusho.

      Maumbo hayo ya udongo yanaonyesha kwamba kwa wazi meli za mapema zilitumiwa kwa shughuli zenye amani za biashara. Meli ndogo ziliendeshwa na wanaume 20 ambao walipiga makasia. Meli kubwa zilitengenezwa ili kusafirisha bidhaa na abiria ambao walitaka kwenda kwenye maeneo ya karibu kandokando ya pwani ya Saiprasi. Plini Mkubwa anasema kwamba Wasaiprasi waliunda meli nyepesi ambayo iliendeshwa kwa makasia ambayo ingeweza kubeba uzito wa tani 90.

      Halafu kulikuwa na meli kubwa za biashara kama ile iliyopatikana karibu na pwani ya Uturuki. Baadhi ya meli hizo zingeweza kubeba mizigo yenye uzito wa tani 450. Idadi ya waliopiga makasia katika meli kubwa ingefikia wanaume 50, wanaume 25 wakiwa kila upande, na meli hiyo ingekuwa na urefu wa mita 30 na mlingoti wenye urefu wa mita 10.

  • “Meli za Kitimu” Zatawala Baharini
    Mnara wa Mlinzi—2007 | Oktoba 15
    • Huenda meli za kivita za mapema zaidi za Saiprasi zilikuwa katika mchoro uliopatikana huko Amathus. Meli hiyo ni nyembamba na ndefu nayo ina tezi iliyoinuka na kujipinda kuelekea ndani ya meli, kama meli ya vita ya Foinike. Ina mdomo wa kutoboa meli ya adui na ngao za mviringo pande zote mbili za tezi na kuelekea omo ya meli hiyo.

Maktaba Kwenye Mtandao (1980-2025)
Toka
Ingia
  • Kiswahili
  • Shiriki
  • Mapendezi
  • Copyright © 2025 Watch Tower Bible and Tract Society of Pennsylvania
  • Masharti ya Utumiaji
  • Sera ya Faragha
  • Mpangilio wa Faragha
  • JW.ORG
  • Ingia
Shiriki