-
Wenye Kufariji UnaokuhusuUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
c Koreshi Mkuu Zaidi, ambaye mwaka wa 1919 aliwakomboa “Israeli wa Mungu” kutoka utekwa wa kiroho, si mwingine ila Yesu Kristo, aliyeketi akiwa Mfalme mtawazwa wa Ufalme wa kimbingu wa Mungu, tangu mwaka wa 1914.—Wagalatia 6:16.
-
-
Wenye Kufariji UnaokuhusuUnabii wa Isaya II—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
Mkombozi Aitwa
6. Nabii anamfafanuaje mshindi wa wakati ujao?
6 Kupitia Isaya, Yehova anatabiri mshindi atakayeokoa watu wa Mungu kutoka Babiloni na pia ahukumu adui zao. Yehova anauliza hivi : “Ni nani aliyemwinua mmoja atokaye mashariki, ambaye katika haki amemwita mguuni pake? ampa mataifa mbele yake, na kumtawaza juu ya wafalme [“kumfanya aende akitiisha hata wafalme,” “NW”]; awatoa wawe kama mavumbi kwa upanga wake, kama makapi yaliyopeperushwa kwa upinde wake. Awafuatia, apita salama hata kwa njia asiyoikanyaga kamwe kwa miguu yake. Ni nani aliyetenda na kufanya jambo hilo, aviitaye vizazi tangu mwanzo? Mimi, BWANA, wa kwanza na wa mwisho, mimi ndiye.”—Isaya 41:2-4.
7. Ni nani mshindi anayekuja, naye anatimiza nini?
7 Ni nani aliyeinuliwa kutoka sehemu za mashariki? Nchi za Umedi-Uajemi na Elamu ziko mashariki ya Babiloni. Koreshi Mwajemi apiga miguu kutoka huko pamoja na majeshi yake hodari. (Isaya 41:25; 44:28; 45:1-4, 13; 46:11) Ingawa Koreshi si mwabudu wa Yehova, yeye anatenda kupatana na mapenzi ya Yehova, yule Mungu mwenye haki. Koreshi anatiisha wafalme, nao wanatawanywa kama vumbi mbele yake. Anafuatia ushindi kwa kupita “salama” katika njia zisizopitiwa kwa kawaida, akishinda vipingamizi vyote. Kufikia mwaka wa 539 K.W.K., Koreshi afikia jiji hodari la Babiloni na kulipindua. Basi watu wa Mungu wanafunguliwa ili warudi Yerusalemu kuanzisha upya ibada safi.—Ezra 1:1-7.c
-