-
Prague Jiji Lenye Historia ya KuvutiaAmkeni!—2003 | Novemba 8
-
-
Unapotembea huku na huku na kustaajabia mandhari, utafika kwa ghafula kwenye Eneo la Kati la Mji wa Kale, na utaona kwanza umati ukikodolea macho saa fulani, hasa inapokaribia kugonga. Hiyo ndiyo Saa ya Baraza la Mji, saa ya falaki yenye kuvutia. Lakini usitarajie ionyeshe mizunguko ya sayari kwa usahihi. Ilitengenezwa wakati watu walipoamini kwamba dunia ilikuwa katikati ya ulimwengu na kwamba jua na nyota ziliizunguka. Hata hivyo, saa hiyo imeundwa kwa njia maridadi na kwa uhandisi wa hali ya juu.a—Ona sanduku kwenye ukurasa unaofuata.
-
-
Prague Jiji Lenye Historia ya KuvutiaAmkeni!—2003 | Novemba 8
-
-
[Sanduku/Picha katika ukurasa wa 23]
Saa ya Falaki
Saa hiyo ina sehemu tatu. Saa inapogonga, madirisha mawili yaliyo upande wa juu hufunguka na kumruhusu mtu aone mifano ya mitume 12 wakifuatana. Mahali pa Yuda Iskariote na Yakobo mwana wa Alfayo pamechukuliwa na Paulo na Barnaba ambao si kati ya wale mitume 12 wanaotajwa katika Biblia. Chini tu ya mitume kuna gofu la mtu, ambalo linawakilisha Kifo. Gofu linapita kwanza kisha linafuatwa na mitume. Gofu linainua na kuinamisha shisha kwa mkono wa kushoto. Mifano mingine inayofuata inatia ndani jogoo anayewika, Mturuki akitikisa kichwa, Ubatili akijitazama kwenye kioo, na Mchoyo ambaye ni mkopeshaji mwenye pupa.
Saa hiyo ya falaki inaonyesha pia aina tatu za wakati—wakati wa Wabohemia katika namba za Kiarabu, wakati wa kawaida katika namba za Kiroma, na wakati wa mchana wenye saa 12 kulingana na mfumo wa Kibabiloni. Sasa unaona umuhimu wa kuichunguza kwa makini saa hiyo maridadi!
-