-
Yehova Mungu Awarehemu MabakiUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
19 Hapo mwanzoni Isaya aliwakemea “binti za Sayuni,” ambao ufisadi wao wa kiadili ulifichwa ndani ya mapambo yao ya kujionyesha. Pia alifichua hatia ya damu ya watu hao kwa jumla, akiwasihi wajioshe. (Isaya 1:15, 16; 3:16-23) Ingawa hivyo, hapo yeye atazamia wakati Mungu mwenyewe atakapokuwa “ameuosha uchafu,” au takataka ya kiadili, na “kufuta madoa ya damu.” (Isaya 4:4, BHN) Utakasaji huo utatekelezwaje? Kwa “roho ya hukumu” na kwa “roho ya kuteketeza.” Uharibifu wa Yerusalemu unaokuja na uhamisho huko Babiloni zitakuwa mfoko wa hukumu za Mungu na hasira kali yake juu ya taifa lisilo safi. Mabaki wanaookoka majanga hayo na kurudi nyumbani watakuwa wamenyenyekezwa, wamesafishwa. Hiyo ndiyo sababu watakuwa watakatifu kwa Yehova na kupata rehema.—Linganisha Malaki 3:2, 3.
-
-
Yehova Mungu Awarehemu MabakiUnabii wa Isaya I—Nuru kwa Wanadamu Wote
-
-
18, 19. Kulingana na Isaya 4:4, 5, ni utakasaji gani atakaotekeleza Yehova, nao utatimizwaje?
18 Kisha Isaya aonyesha jinsi wakazi wa nchi iliyorudishwa watakavyokuwa watakatifu na baraka watakazopata. Asema: “Hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza.
-