-
Yerusalemu Katika Nyakati za Biblia—Akiolojia Yafunua Nini?Mnara wa Mlinzi—1997 | Juni 15
-
-
Mathalani, Daudi aliwaambia wanaume wake kwamba “yeye atakayewapiga Wayebusi, na apande kwenye mfereji wa maji, [na akutane]” na adui. (2 Samweli 5:8) Yoabu kamanda wa Daudi alifanya hivyo. Msemo “mfereji wa maji” wamaanisha nini hasa?
-
-
Yerusalemu Katika Nyakati za Biblia—Akiolojia Yafunua Nini?Mnara wa Mlinzi—1997 | Juni 15
-
-
Kwa muda mrefu wasomi wametambua kwamba chanzo kikuu cha maji ya jiji la kale kilikuwa chemchemi ya Gihoni. Kilikuwa nje ya kuta za jiji lakini karibu vya kutosha kuruhusu mtaro na shimo lenye urefu wa meta 11 kuchimbuliwa, ambao ungewezesha wakazi wachote maji bila kwenda nje ya kuta zenye kinga. Hilo lilijulikana kuwa Warren’s Shaft, likiitwa kwa jina la Charles Warren ambaye alivumbua mfumo huo katika mwaka wa 1867. Lakini mtaro na shimo vilifanyizwa lini? Je, vilikuwako wakati wa Daudi? Je, mtaro huu wa maji ulitumiwa na Yoabu? Dan Gill hujibu: “Ili kujaribu kama Warren’s Shaft lilikuwa kwa hakika shimo la asili, tulichunguza ganda la kipande cha chokaa kutoka kuta zalo zisizo laini ili kupata carbon-14. Halikuwa na kitu, hilo likionyesha kwamba ganda hilo lina miaka zaidi ya 40,000: Hilo latoa uthibitisho ulio wazi kwamba hilo shimo halingaliweza kuwa lilichimbwa na mwanadamu.”
-